loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

KAM kujenga hospitali ya mafunzo

Hayo yalisemwa juzi na Mkuu wa chuo hicho, Dk Kandore Musika, wakati akielezea madhumuni ya kuanzisha chuo hicho na mahafali yatakayofanyika Kimara jijini Resort Dar es Salaam kesho.

Alisema hivi sasa wanafunzi wanaohitimu chuoni hapo wanafanya mafunzo kwa vitendo katika hospitali za Manispaa ya Ilala, Temeke na Kinondoni na mikoa ya Pwani hivyo lengo la sasa ni kuwa na hospitali ya mafunzo ya KAM.

Alisema mbali na upungufu mkubwa wa madaktari bingwa, wataalamu wengine kama fundi maabara, wauguzi na wafamasia pia idadi yao haitoshi na vyuo vinavyotoa mafunzo ya taaluma hizo ni vichache hapa nchini.

“Kutokana na changamoto hizo serikali imetoa uhuru kwa watu binafsi kuanzisha vyuo vya sayansi ya afya na tiba na moja ya taasisi kizalendo zilizoitikia mwito huo haraka ni KAM DSM Pharmacy Ltd ambayo imeanzisha chuo kuongeza idadi ya wataalamu wa afya,” alisema Dk Musika ambaye pia ni Mwenyekiti na Mwanzislishi wa muungano wa vyuo binafsi vya afya Tanzania APHECOT.

Alisema wakati mipango kabambe ya kujenga hospitali hiyo kubwa ya mafunzo ikiendelea, chuo cha KAM kitaendelea kuimarisha na kudumisha ushirikiano uliopo baina yake na hospitali za Manispaa za Dar es Salaan, Tumbi na Kisarawe.

Alisema wataendeleza ushirikiano wa kitaaluma na vyuo vingine Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na mashirika mbalimbali ya kimataifa.

Dk Musika alisema chuo chake kitasimamia majukumu halisi ya kutoa taaluma katika kiwango cha juu katika mazingira mazuri na watalamu wa kutosha na wenye sifa stahili katika ngazi ya shahada na stashahada.

WAZIRI wa Maendeleo ya Nishati na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi