loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kama Mzazi: Kamwe tusihalalishe ngono kwa wasichana

Ni wasichana wanaojiuza miili yao katika mitaa ya mji wa Tanga, barabara ya Independence na bustani ya mapumziko ya Forodhani. Ni kama vile mteja anavyoulizia bei ya bidhaa fulani akachagua ipi anataka na kwa bei anayoweza kulipia. Hebu fikiria bei zenyewe.

Huduma ya haraka Sh 2,000 tena papo hapo, kinyume cha maumbile Sh 5,000 na Sh 10,000 ndani ya gari! Hayo siyo yangu jamani ni ya watu wanaoshuhudia senema hii kila siku mjini Tanga, nyakati za usiku.

Mashuhuda wetu kama walivyo wapelelezi walisema waliona msichana akivua nguo na kumwonyesha mteja mwili wake akitamba, “Nitazame mimi sina kovu hata moja mwilini.” Ni nguvu ya kuvutia wateja wake aliyonayo. Ni kazi kubwa kwelikweli.

Lakini hivi tumeshafikia kiasi hiki cha kutojali kabisa utu wetu, ustaarabu wetu, utamaduni wetu na hadhi zetu kama binadamu tena waafrika wenye mila na desturi maridhawa zenye kusifika na kutukuka duniani kote?

Mambo hayo yanafanywa ndani ya jamii yetu huku tukishuhudia. Hivi ni kweli kwamba hatuwezi kufanya lolote kudhibiti hali hiyo isiweze kuenea kwa kasi kiasi cha kuhalalisha kuwa shughuli halali ya kujipatia kipato?

Sote tunafahamu magonjwa yanayotokana na vitendo hivi, ukiwemo Ukimwi? Mimi siamini kwamba wasichana hao kweli wameshindwa kutafuta njia mbadala ya kujipatia kipato halali cha kati ya Sh 2,000 hadi 10,000 wanazosaka kwa wateja kwa njia hii dhalimu.

Ngono hadharani na kwenye magari! Tena kwa mtindo huu hakuna hata cha kutumia mipira ya kondomu kujikinga na maradhi hususani Ukimwi. Hivi tunaelekea wapi kwa mtindo huu?

Sitaki niamini kwamba hayo yanafanyika halafu vyombo vya dola havina habari. Hivi kama raia wa kawaida tu anashuhudia hayo, iweje vyombo vya dola na uwezo wa mafunzo na uzoefu walionao washindwe kuliona hili?

Watumishi wa vyombo vya dola, viongozi wa dini, wazazi na walezi tuko wapi kulidhibiti hili ovu? Hali ya ngono zembe inayofanywa mjini Tanga na wasichana wadogo inawezekana ipo pia katika miji mingine mikubwa hapa nchini.

Miji yote mikubwa, ikiwa ni pamoja na manispaa na majiji yetu yana viongozi wa ngazi mbalimbali ambao wanaweza kulisimamia na kulidhibiti jambo hili hatari ili lisiendelee kufanyika kama vile ni sawa na shughuli halali ya kujipatia kipato.

Mbona katika jiji la Dar es Salaam wakati mwingine polisi huendesha operesheni ya kukamata wazururaji na wanaojiuza miili yao? Kwa nini hili wenzetu wa Tanga wasilichukue pia kukabili hali hiyo ya aibu? L

akini tumeambiwa kwamba wakati upande mmoja wa shilingi kuna wasichana wanaouza miili yao, vijana wanawaita ‘machangudoa’, upande mwingine kuna wanunuzi wa huduma hiyo, ‘machangupapa’.

Bila shaka vita hii inapaswa pia iwalenge machangupapa. Wakikamatwa wachukuliwe hatua na kutangazwa hadharani kwa sababu kama hakuna wanunuzi, hakuna biashara! Naamini hatujachelewa.

Viongozi wote ndani ya mji maarufu wa Tanga wakusanye nguvu zao kulikabili na kulidhibiti jambo hili lisijegeuzwa kuwa shughuli halali ya watoto wetu wa kike. Penye nia pana njia.

UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Riadha ...

foto
Mwandishi: Nicodemus Ikonko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi