loader
Picha

KAMA MZAZI: Tukatae filamu, video za ngono kwenye mabasi

Ukiacha buradani hiyo, wasafi ri pia walikuwa wanaburudishwa na kanda za video za muziki, michezo ya kuigiza na fi lamu za Bongo. Hapa ndipo palipomgusa Kama Mzazi kutokana na picha zilizokuwa zinashuhudiwa kwenye video hizo.

Kuanzia muziki, maigizo na fi lamu hizo, sehemu kubwa zimejikita katika masuala ya ngono ambayo katika hali ya kawaida hazipaswi kuruhusiwa kuoneshwa katika muktadha wa usafi ri wa umma.

Niliyokuwa nayashuhudia yalinikumbusha umuhimu wa Bodi ya Filamu kuchukua hatua stahiki ya ukaguzi wa kina kwa video za muziki, michezo ya kuigiza na fi lamu ili kudhibitiwa kuoneshwa katika usafi ri wa umma kama huo.

Hakuna ubishi kwamba usafi ri wa mabasi ya umma hujumuisha watu mbalimbali wa familia moja na wenye mahusiano ya kijamii ikiwa ni pamoja na baba, mama, wakwe, shangazi, wajomba, vijana wa kiume na wa kike walio wadogo kwa wakubwa na wengine wengi.

Mkusanyiko wa aina hii nao unahitajika kufi kiriwa kwa umakini unaostahiki ili kuwezesha wasafi ri husika wasafi ri kwa raha badala ya kuwekwa katika hali za kuwapatia burudani ambayo kwa kiasi kikubwa inaongozwa masuala ya ngono. Burudani ya aina hii inakuwa kama adhabu kwa abiria wenye kusafi ri na familia zao.

Katika kutoa burudani ndani ya mabasi ya usafi ri wa umma, wahusika wakiwemo makondakta na madereva wafi kirie pia kulinda mila, desturi na tamaduni zetu za Kiafrika ambazo masuala ya ngono ni masuala nyeti hayapaswi kuoneshwa hadharani mchana kweupe na kwenye hadhara mchanganyiko wa aina hiyo.

Kama Mzazi haipingani na dhana ya kuburudisha wasafi ri ndani ya mabasi lakini pia aina ya burudani iendane na kuzingatia mchanganyiko wa wasafi ri kwa kulinda mila na desturi zetu.

Katika hili Kama Mzazi inapenda kuwakumbusha wahusika wote katika masuala ya usafi ri wa umma kwenye mabasi na njia nyingine za usafi ri kuweka burudani kulinda hadhi na tamaduni zetu badala ya zile za kukuza masuala ya ngono moja kwa moja.

Inawezekana pia kutakuwa na watu watakaopinga hilo kwa madai kwamba ni haki yao kuburudishwa na burudani ya aina hiyo lakini pia kwa mtindo huu kama ukiachiwa kuendelea kama ulivyo, tutaua mila na desturi zetu ambazo ndizo bado zinatulinda kuendelea kuwa na umoja na mshikamano na kuheshimiana.

Hapa wamiliki wa vyombo vya usafi ri, wafanyakazi wao pamoja na vyombo vinavyohusika na maadili viingilie kati kwa makusudi kudhibiti hali hiyo. Inawezekana kuchukua hatua stahiki bila kufanya ajizi.

JUZI iliibuka taarifa katika mitandao ya kijamii juu ...

foto
Mwandishi: Nicodemus Ikonko

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi