loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kama Mzazi: Watoto kufunzwa maadili ni muhimu

Mwenye kushika maadili huwa ni mtiifu, makini, mchapakazi, hodari na pia huwa ni kipenzi cha watu. Lakini maadili hayo yanapatikanaje na kwa nini hivi sasa yanapewa kisogo na vijana wetu wa kike na kiume?

Kubwa na la msingi hapa ni suala la malezi wanayopata watoto wetu kutoka kwa wazazi au walezi wao. Napenda kukiri kwamba mimi si mwanataaluma katika malezi lakini ni ukweli kwamba taasisi za dini zina dhima kubwa katika mafunzo ya maadili kwa watoto wetu.

Katika hali ya kawaida huko tunakoishi mijini na vijijini wazazi na walezi makini, mbali na wao kusimama imara katika kutoa malezi mema, pia huwapeleka watoto wao katika mafunzo ya maadili kupitia dini zao.

Kwa mfano wenzetu wa Kikristo huwa na vipindi vya dini kwa watoto kanisani na kwa upande wa Waislamu hupeleka watoto wetu kwenye madrasa.

Huhitaji kuwa na elimu ya ziada kugundua tofauti kati ya watoto wanaopitishwa katika utaratibu wa aina hii na wale ambao huwakubahatika kufuata mifumo ya aina hii.

Tofauti hizo pia hujionesha wazi unapolinganisha na maisha ya watoto wa mitaani au watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Watoto wa aina hii kwa bahati mbaya huwa hawana nafasi ya kuhudhuria katika mafunzo ya maadili kama nilivyotaja hapo juu.

Matokeo yake hukosa unyenyekevu, utulivu, kutenda mambo mema na hujitumbukiza katika vitendo vya uhalifu kama vile udokozi, wizi na hatimaye katika utu uzima ndiyo hujikuta katika ujambazi.

Kama Mzazi katika safu yetu wiki hii napenda kuwakumbusha wazazi na walezi wengine kuzingatia umuhimu wa kuwaongoza watoto wetu katika taasisi zetu za dini ili viongozi wetu wa dini wachukue nafasi yao ya kiroho kuweza kuwapatia mafunzo ya kuwaweka sawa kimaadili.

Hivi kwa mfano zisingekuwepo taasisi za dini mbalimbali katika jamii yetu na kwamba watoto tangu wazaliwe wanakua tu bila kujua kanisani, msikitini au eneo lolote lile la ibada, hali ingekuwaje.

Hata wakati ule kabla ya ujio wa dini hizi mbili na nyingine hapa nchini, mababu zetu walikuwa pia na aina fulani ya dini zao ambazo zilikuwa zinawaongoza katika kuwasiliana na Mungu kwa maana ya maombi yao mbalimbali-kutambika.

Kwa bahati mbaya moto wa watoto wa kizazi chetu hiki cha dotikomu umepoa mno juu ya kushiriki katika ibada mbalimbali na matokeo ya hali hiyo ni kukosekana maadili na nidhamu, hali ambayo sote tunaishuhudia lakini hakuna juhudi za makusudi za kurejesha umuhimu huo katika jamii yetu.

Sitaki niami kwamba tumechelewa bali bado tunayo nafasi ya kurekebisha hali hiyo inayotishia jamii yetu kwenda mrama katika suala zima la maadili kwa kuchukua hatua za kurejesha watoto wetu katika maadili mema ya dini zetu.

Naamka asubuhi,  sioni kilongalonga, 
Napapasa kitandani,  hamadi hiki hapa,  

foto
Mwandishi: Nicodemus Ikonko

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi