loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kambi Maisha Plus kuanza Machi 16

Ofisa Kampeni, Ushawishi na Utetezi wa Oxfam, ambao wanaendesha shindano hilo, Mkamiti Mgawe alisema washiriki 45 watachuana kuwania Sh milioni 25 katika Maisha Plus.

Mgawe alisema pia wakulima akinamama nao watachuana katika shindano la kuwania vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Sh milioni 20.

Wakati vijana wa Maisha Plus wataingia kambini baada ya kupigiwa kura na wanavijiji, wenzao wa Mama Shujaa wa Chakula watapigiwa kura katika mitandao ili kuwapata washiriki 20 watakaochuana kusaka mshindi.

Mwaka jana, mshindi wa Maisha Plus aliondoka na Sh milioni 20 huku Mama Shujaa wa Chakula aliondoka na vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Sh milioni 15.

Alisema tofauti na mwaka jana, mwaka huu washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula watakaofikia fainali, kila mmoja ataondoka na kifuta jasho wakati mwaka jana kifuta jasho hakikuwepo.

KLABU ya Chelsea imemtangaza ...

foto
Mwandishi: Cosmas Mlekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi