loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Kampuni 19 zafungiwa zabuni

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Marten Lumbanga alisema mbali na kampuni hizo, pia bodi hiyo kupitia kikao chake kilichoketi jana, pia imefikia uamuzi wa kuzisimamisha kwa muda kampuni nne kushiriki katika zabuni hizo hadi pale mchakato wa kuzifungulia utakapoafikiwa.

Alizitaja baadhi ya kampuni hizo kuwa ni pamoja na M/s Quality Motors Limeted, M/s Agumba Computers,M/s Chanuo Store, M/s Rulendi Women Group, M/s Apico Tanzania Limited, M/s Bamingo Construction C Limited, M/s Designer Limited, M/s New Century Construction Co Limited, M/s V.R.B Construction Co. Limited na zingine 10.

Alisema hatua hiyo imebainika kutokana na ukaguzi uliofanyika kipindi cha mwaka 2013/2014 katika maeneo mbalimbali zikiwemo wizara, idara zinazojitegemea, wakala za serikali 17, mamlaka na mashirika ya umma 16 pamoja na serikali za mitaa 46.

Aidha Balozi Lumbanga alisema ukaguzi wa thamani ya fedha uliofanywa kwa taasisi 45 kati ya 68 kwa kuhusisha miradi 205 yenye jumla ya Sh bilioni 62.5, ikiwemo 90 ya ujenzi wa barabara, 53 ya majengo,33 ya usambazaji wa maji, 16 madaraja, 2 ya umwagiliaji, 10 ya mabwawa na moja ya huduma za ushauri, ulionesha udhaifu katika usimamizi na utekelezaji wa mikataba.

Alisema udhaifu huo ulichangia ucheleweshaji wa huduma,kuongezeka kwa gharama katika mikataba, ubora hafifu wa huduma, vifaa na kazi za ujenzi na upotevu wa pesa za serikali kwa kufanya malipo hewa na sababu nyinginezo.

“Pia kupitia ukaguzi huo kumebainika udhaifu katika usimamizi wa mikataba ya ukusanyaji wa ushuru kwenye Serikali za Mitaa, katika mikataba ya ukusanyaji ushuru 146 iliyokaguliwa, Sh bilioni 2.7 ambazo ni sawa na asilimia 32.5 ya Sh. bilioni 8.3 zilizotakiwa kukusanywa hazikuweza kukusanywa bila sababu,” alisema Lumbanga.

Pia alisema ukaguzi wa thamani ya fedha uliofanywa katika miradi 205 ya ujenzi, iliyooneshwa ni miradi 33 yenye thamani ya Sh bilioni 18.5 sawa na asilimia 16.1 ya miradi yote. Alisema miradi hiyo ilitekelezwa kikamilifu kwa mujibu wa mikataba licha ya kuwapo kwa upungufu mdogo mdogo ambao taasisi husika zilitakiwa kuzirekebisha.

Aidha alisema Bodi ya Wakurugenzi ya PPRA imeiagiza Menejimenti ya PPRA kufanya uhakiki wa taarifa za kuwepo kwa malipo ya ziada kwa kazi kwa taasisi ambazo hazikufanyiwa uamuzi ili bodi iweze kufanya uamuzi stahiki.

KAMPUNI ya Vodacom Tanzania imetangaza ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi