loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kampuni ya mafuta yazindua vilainishi

Akizungumza kwenye uzinduzi wa vilainishi hivyo vya magari jana katika kituo kipya cha mafuta ya Oysterbay jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo nchini, Phillipe Corsaletti alisema promosheni hiyo itafanyika kwa wiki kadhaa.

“Castrol inaongoza duniani katika ubora wa utengenezaji, usambazaji, matangazo ya vilainishi, grisi na huduma zinazohusiana na bidhaa hizo zitumikazo katika magari, viwanda, meli, ndege na katika uchunguzi na uchimbaji wa mafuta ghafi. “Puma na Castrol tuna mkakati wa pamoja na malengo sawa ya kukuza biashara yetu katika maeneo mbalimbali barani Afrika. Hivyo tega masikio na chunguza kwa makini alipo ‘Puma Man’ na ulizia ofa maalumu ambazo tunazitoa kwenye bidhaa zetu za Castro GTX 20W50 & GTX Diesel 15W40, katika kipindi hiki cha uzinduzi,” alisema Corsaletti.

Puma Energy ni moja ya kampuni inayokua kwa kasi duniani, ikijishughulisha na usafirishaji, usambazaji wa mafuta vituoni na kwa watumiaji wakubwa wa mafuta. Puma Energy inafanya kazi zake katika nchi za Mashariki ya Kati, Afrika, Ulaya, na Amerika ya Kusini.

Puma ilianzishwa mwaka 1997 ikiwa na lengo la kuanzisha mtandao mkubwa unaojitegemea wa kuhifadhi na kusambaza bidhaa za mafuta. Puma ipo katika nchi zaidi ya 35 duniani likiwa na ofisi za kanda katika nchi za Afrika Kusini, Singapore, Australia na Estonia.

Puma Energy inatoa ajira kwa zaidi ya watu 6,000 duniani na wengine zaidi ya 20,000 wakipata ajira katika vituo vya mafuta.

Trafigura Group ambao ni miongoni mwa wachuuzi wakubwa wa bidhaa mbalimbali duniani, wanamiliki asilimia 50 ya hisa za Puma Energy. Sonangol kampuni ya mafuta inayomilikiwa na serikali ya Angola inamiliki asilimia 30 ya hisa za Puma Energy.

Asilimia 50 ya hisa za Puma Energy Tanzania zinamilikiwa na Serikali ya Tanzania, wakati asilimia 96 ya wafanyakazi wake 154 ni Watanzania wazawa. Aidha inatengeneza ajira kwa takribani watu 405 wanaofanya kazi kwenye vituo vya mafuta.

KAMPUNI ya uchimbaji ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi