Mchangiaji anatakiwa kutuma neno MAAFA kwenda namba 15626 . Ujumbe huu utalipiwa Sh 256 na pesa hiyo itaingia kwenye mfuko wa kuchangia waathirika wa mafuriko mkoani Shinyanga.
Taarifa hiyo wameitoa jana wakati walipowatembelea waathirika wa mafuriko ya mvua katika wilaya ya Kahama mkoani shinyanga na kuwapatia msaada wa mahitaji muhimu Zaidi ya watu 35 walikufa katika janga hilo ambalo liliacha mamia ya watu bila makazi.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya msaada huu, Meneja Mauzo wa Airtel Shinyanga Ezekiel Nungwi alisema taasisi hiyo inaungana na taifa katika kutoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao na marafiki na wanafamilia kutokana na mafuriko hayo.
“Tunatambua pia mafuriko haya yamewaacha wakazi wengi bila makazi, huku mazao yao kuharibiwa na mifugo yao kufa hivyo tunaungana kwa pamoja kutoa msaada kwa namna tutakayoweza , “ alisema.
Katika hafla hiyo Airtel wametoa msaada wa mabati, mablangeti, magodoro pamoja na chakula vyenye thamani ya Sh milioni 3 na kuwaomba Watanzania kuungana nao ili kuepuka milipuko ya magonjwa isitokee na kuwawezesha kurudi kufanya shughuli zao za kawaida mapema iwezekanavyo.
Akizungumza kwa niaba ya wakazi wa Kahama Mkuu wa Wilaya Benson Mpesya amewashukuru Airtel kwa kuwakumbuka wananchi wa Kahama na kuomba misaada zaidi ili kukabili changamoto zilizopo wilayani humo.