loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kampuni yaanzisha huduma kwa wajasiriamali

Kampeni hiyo ina lengo la kuwawezesha wajasiriamali wa Tanzania kutangaza bidhaa zao na hivyo kujiinua kiuchumi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Edwin Bruno alisema hatua hiyo, imelenga kutambulisha biashara ya mjasiriamali huyo kitaifa na kimataifa.

Alisema huduma ya ‘Patikana’ inayomwezesha kila mfanyabiashara kujitangaza kupitia teknolojia ya tovuti, pia itamfanya kuwa na jina lake litakalotambulika kibiashara na hivyo kumfanya ajulikane duniani.

“Kutokana na kukua kwa teknolojia, siku hizi wafanyabiashara wamekuwa wakipoteza wateja wengi wanaowatafuta mtandaoni kutokana na kutokuwa na website zinazoonesha huduma wanazozitoa jambo lililotufanya tuanzishe huduma hii ya PATIKANA ili kukidhi matakwa yao hayo,” alisema Bruno.

Aidha, alisema kampuni ya Smart Codes iliyoanzishwa mwaka 2010 hadi sasa imeshatoa huduma ya aina hiyo na zingine nyingi zinazohusu masuala ya mtandao kwa makampuni mbalimbali ya hapa nchini bila tatizo lolote, jambo linalowafanya kujivunia.

Alisema kampuni hiyo iliyoanzishwa na vijana wa Tanzania, walioamua kujiajiri katika utoaji wa huduma hiyo, itahakikisha inatoa msaada kwa wajasiriamali wote wadogo na wakubwa bila upendeleo kwa nia ya kuwawezesha kutimiza malengo yao.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi