loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kampuni yalipa milioni 800/- kutafiti gesi

Kampuni hiyo, Altus Oilfield Services FPZ ya Singapore imetoa hundi ya dola za Kimarekani 526, 280 sawa na Sh milioni 800 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa miundombinu ya eneo hilo.

Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, Dk Adelhelm Meru aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati wa kupokea hundi hiyo kuwa fedha hizo zitatumika kuanza kujenga miundombinu ya msingi kama barabara, umeme, maji na njia ya maji taka katika eneo la kampuni hiyo.

“Uwekezaji katika eneo hilo utasaidia kukuza ajira na uchumi wa nchi kuimarika zaidi,” alisema.

EPZA inaendeleza hekta 10 za eneo huru la Bandari ya Mtwara. Mwakilishi wa Kampuni ya MAC Group Limited aliyekabidhi hundi hiyo, Nagarayan Sankaranarayanan alisema kampuni yake imejiandaa kuanza kufanya kazi ya kutoa huduma kwa kampuni za utafutaji gesi na mafuta.

Eneo hilo ni kati ya hekta 110 za eneo hilo huru la bandari ambalo limetengwa na serikali kwa ajili ya uwekezaji mbalimbali.

Hekta hizo 10 zitaendelezwa kwa kuwekewa miundombinu inayotakiwa na kisha kugawiwa kwa kampuni za kimataifa zinazofanya kazi za kutoa huduma mbalimbali kwa kampuni zinazofanya utafiti wa mafuta na gesi katika Mkoa wa Mtwara.

Imeelezwa kituo hicho cha huduma kwa kampuni zinazofanya utafiti, kitakapokamilika kitakuwa cha kipekee si kwa Tanzania pekee, bali katika ukanda mzima wa Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Kampuni nyingine zilizoingia Mkataba na EPZA mwezi uliopita kuwekeza katika eneo hilo, ni Slumberger Seaco Inc ya Marekani, Tans Ocean Industries and Services LTD ya Dubai na Lenna ya Iran.

Kazi ya kupata wawekezaji katika eneo hilo, ilianza mwaka 2010 baada ya kampuni za utafutaji gesi na mafuta kuomba kuwepo kwa kampuni za watoa huduma.

Miongoni mwa vitu vitakavyokuwepo katika eneo hilo, ni karakana kubwa kwa ajili ya kufanyia ukarabati na matengenezo ya vifaa vya mafuta na gesi.

Karakana hizo zitajengwa kisasa na zitakuwa na uwezo pia wa kuhudumia nchi jirani kama vile Kenya, Msumbiji, na Afrika Kusini. 

SERIKALI imesema inatoa bei halali ya madini inayonunua kutoka kwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi