loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kanda ya Ziwa kiboko Umitashumta

Ziwa juzi walitisha katika mchezo wa kuruka chini kwa upande wa wasichana na wavulana baada ya kutwaa medali nne katika mchezo huo.

Kwa upande wa mbio za mita 200 wasichana; Christina Pascal wa Kanda ya Ziwa aliibuka wa kwanza na kuondoka na medali ya dhahabu baada ya kumaliza mbio hizo kwa kutumia sekunde 26:93 huku nafasi ya pili ikienda kwa Neema Eliya wa Mashariki aliyemaliza kwa sekunde 26:00.

Kanda ya Ziwa iliendeleza makali yake katika riadha baada ya wachezaji wake wawili Amani aboubakar na Baraka Bitulo kushika nafasi ya kwanza na pili katika mbio za mita 200 kwa wavulana kwa kutumia sekunde 23:38 na 24:97 wakati Mohamed Idd wa Kati akimaliza wa tatu kwa sekunde 24:98.

Ziwa waliendelea kuzoea medali katika riadha baada ya wanariadha wake wawili, Sarah Joel na Agnes Frank kushika nafasi mbili za kwanza katika mita 400 kwa wasichana na kuzoa dhahabu na fedha.

Katika mbio hizo, Edna Chipolo wa Mashariki alipata medali ya shaba akiwa wa tatu kwa kutumia dakika 1:02.56 wakati kwa wavulana nafasi tatu za kwanza zilichukuliwa na na Kusini, Kati na Ziwa Magharibi.

Katika mchezo wa kurusha kisahani; Sakina Ngalo wa Nyanda za Juu aliibuka mshindi baada ya kurusha umabli wa mita 20 na sentimeta 46 kwa upande wa wasichana huku Hellen Gitali wa Kaskazini Magharibi akishika nafasi ya pili kwa kurusha mita 20.29.

Kisahani kwa wavulana; Joel Joseph wa Kaskazini Magharibi alimaliza wa kwanza kwa kutupa umbali wa mita 26 na sentimeta 40 huku Yona Mwakibibi wa Nyanda za Juu akishika nafasi ya pili na ile ya tatu ikienda kwa Charles Masanja wa Ziwa Magharibi.

Katika mpira wa wavu; Nyanda za Juu waliibuka wababe baada ya kuwasambaratisha Kanda ya Dar es Salaam kwa seti 3-0 huku washindi wakishinda wavulana kwa 25-14, 25-15 na 25-14.

MBIO ya Tanzania Women ...

foto
Mwandishi: Cosmas Mlekani, Kibaha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi