loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kashfa yanyemelea Jiji la Arusha

Habari zilizopatikana kutoka katika kikao cha Kamati ya Fedha na Uchumi cha Jiji la Arusha kilichokaa Agosti 29, zimeeleza kuwa wajumbe wa kamati hiyo, walimwomba Mkurugenzi wa Jiji, Juma Iddy, kutoa taarifa za kina ni lini Bodi ya Zabuni ilikaa na kuipa kampuni hiyo (jina tunalo) kazi ya ukusanyaji wa ushuru wa maegesho ya magari.

Taarifa zaidi zinadai kuwa Mkurugenzi alielezwa kuwa kikao cha awali cha Kamati ya Tathmini inayoundwa na wataalamu, kiliamuru kipelekewe maelezo ya kina ya kila kampuni iliyoomba zabuni na baada ya kuyapata na kuyapitia, ilitoa mapendekezo na kurudisha tena katika kikao cha Bodi ya Zabuni kwa uteuzi.

“Maelezo ya kampuni tatu zilizopita mchakato wa awali, yalipelekwa na Kamati ya Tathmini iliondoa kampuni mbili kwa kushindwa kukidhi vigezo katika hatua ya pili, hasa katika kipengele kilichotaka kila mzabuni kuwasilisha taarifa ya fedha ya benki ya kuanzia Juni 2013 hadi Aprili 2014,’’ ilidai taarifa kutoka katika kikao hicho.

Kufuatia hali hiyo, ilielezwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi na Meya wa Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo aliamuru zabuni hiyo kutopitishwa na Kamati hiyo ya Fedha na alimwagiza Mkurugenzi wa Jiji kukusanya vielelezo vyote vilivyotumika kupitisha zabuni hiyo na kuviwasilisha katika kikao kilichokaa juzi kujadili suala hilo.

Zabuni za ukusanyaji mapato ndani ya Jiji la Arusha zilitangazwa Aprili mwaka huu na mwisho ilikuwa Mei 29 mwaka huu.

Washindi wa zabuni walipaswa kuanza kazi Julai Mosi baada ya siku 14 kutolewa kwa mzabuni atakayeona haki haikutendeka, kukata rufaa.

Habari kutoka ndani ya Halmashauri ya Jiji la Arusha, ilieleza kuwa, hivi sasa miezi miwili na nusu imepita tangu wazabuni wapya walipotakiwa kuanza kazi, huku wazabuni waliokuwepo awali wakiongezewa muda wa kuendelea kukusanya ushuru huo.

Ucheleweshwaji wa kupewa barua kwa wazabuni waliokidhi vigezo na kuteuliwa na kamati za zabuni, unadaiwa kufanywa na Katibu wa zabuni wa Jiji la Arusha, Mussa Mbwana, kwa madai ya mgongano wa maslahi.

Akijibu tuhuma hizo kwa njia ya simu yake ya mkononi, Mbwana alisema hawezi kutoa ufafanuzi wa tuhuma hizo mpaka atakapoelezwa mtu aliyetoa habari hizo.

Alipoelezwa mtoa taarifa hatotajwa kwake, alikata simu. Mkurugenzi wa Jiji alipopigiwa simu yake ya kiganjani kuzungumzia tuhuma hizo, alisema yupo safarini Kilimanjaro na kwamba hawezi kujibu chochote juu ya hilo, kwani mambo yaliyojiri kwenye kikao hicho ni siri.

RAIS John Pombe Magufuli anaongoza kwenye ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi