loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Katani yaipa NSSF gawio la milioni 54/

Gawio hilo lilitolewa Jumamosi jijini Dar es Salaam wakati wa semina ya wahariri wa vyombo vya habari nchini, iliyoandaliwa na NSSF.

Akikabidhi hundi ya fedha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa NSSF Dk Ramadhani Dau, Kaimu Mkurugenzi wa Katani Ltd, Juma Shamte alisema katika kipindi cha Mwaka 2006/2013 , NSSF imeshatoa kiasi cha Sh bilioni 14.8 kwa uwekezaji wa katani, ambao unakua kwa kiwango kwa kasi na kuchangia pato la taifa.

Kwa mujibu wa Shamte, uwekezaji huo wa NSSF katika Kampuni ya Katani, umeiwezesha Kampuni kupata faida kubwa, kiasi cha Sh bilioni 13 mwaka jana, na hivyo kuanza kutoa gawio kwa wanahisa wake.

Akizungumza wakati wa kupokea fedha hizo Mkurugenzi Mtendaji wa NSSF, Dk Ramadhani Dau alisema: “NSSF imekuwa na muendelezo wa kuchangia katika uwekezaji wa ndani unaomgusa mwananchi moja kwa moja”.

NSSF, kwa mujibu wa Dau, itaendelea kuwekeza kwenye miradi itakayowanufaisha Watanzania walio wengi zaidi, na kutoa kwa wadau wengine wa maendeleo kuwekeza kwenye miradi kama hiyo ili kuchochea kasi ya maendeleo ya Watanzania na Taifa kwa ujumla.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi