loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Kaya 150 zateketezwa

Inadaiwa zimeteketezwa na wafugaji wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Magogo, Abudallah Mrisho aliwaeleza waandishi wa habari kuwa tukio hilo la kuvamiwa na wafugaji wa Kishapu ni la Novembea 10 mwaka huu, saa 7 mchana.

Alidai wafugaji hao walivamia kitongoji hicho, wakisema eneo hilo ni mali ya mkoa wa Shinyanga na kuwaamuru wakulima kuondoka kisha walichoma na kuharibu mali mbalimbali.

Diwani wa kata hiyo, Dotto Kwirasa aliishutumu Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Igunga kuwa ina udhaifu mkubwa na imesababisha kutokea tena kwa uharibifu huo.

Alisema wamekuwa wakitoa mara kwa mara taarifa za kutaka kuvamiwa, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa hadi ulipotokea uvamizi huo kwa mara ya pili.

Alisema kutokana na tukio hilo, watu 450 hawana makazi na hawana huduma muhimu. Mkuu wa wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu alipotafutwa kwa simu yake, iliita tu bila kupokelewa.

Hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi, haukujibiwa. Ofisa Tawala wilaya hiyo, Alphonce Kasanyi akizungumza kwa simu yake ya mkononi, akiwa safarini Mpanda, alikanusha kuwepo kwa barua iliyothibitisha wafugaji kulima eneo hilo.

Alisisitiza kuwa tuhuma zote dhidi ya ofisi ya Mkuu wa wilaya, sio za kweli. Aliagiza vyombo vya dola vifanye kazi yake kwa mujibu wa sheria.

Wakizungumza kwa nyakati mbalimbali, wakulima hao wameiomba viongozi wa ofisi ya waziri mkuu wawatembelee ili kutatua mgogoro huo, ambao umedumu muda mrefu na kuhatarisha maisha ya wananchi.

WAZIRI wa Maendeleo ya Nishati na ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Tabora

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi