loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kesi ya wafanyakazi Swissport yaahirishwa

Wafanyakazi hao, Daud Mwenga (49) na Jackson Kituka (30) ambao walidaiwa kuiba simu zenye thamani ya Sh milioni 5.2 walifunguliwa mashitaka katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala.

Wakili wa Serikali, Ester Kyala, aliiambia Mahakama kwamba, wakili aliyemtaja kwa jina moja la Jamhuri hakufika mahakamani hapo kwa kuwa yupo Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.

Pia, aliiomba Mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kusikiliza shauri hilo. Hakimu Flora Haule alikubaliana na maelezo hayo na kusema kuwa shauri hilo litasikilizwa Julai 28 mwaka huu.

Awali, kesi hiyo ilikuwa mbele ya Hakimu Janeth Kinyage lakini imehamishiwa kwa Hakimu Haule kutokana na kuhamishwa kikazi kwa Kinyage aliyekuwa anasikiliza shauri hilo.

Ilidaiwa kuwa Novemba 11 mwaka jana, maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Wilaya ya Ilala, washitakiwa wanadaiwa kuiba simu zenye thamani ya Sh milioni 5.2, mali ya Sued Chemchem.

Washitakiwa walikana na wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti waliyotakiwa.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi