loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kibo Gold Lager yatwaa medali ya dhahabu

Kibo ilipokea utambulisho huo wa kimataifa wakati wa sherehe za 53 za kila mwaka zilizofanyika Bordeaux, Ufaransa.

Tuzo hizo huendeshwa na Kampuni ya Biashara ya nchini Ubelgiji ambayo hujihusisha na ubora. Bidhaa huonjwa na kujaribiwa ziweze kupewa alama ya ubora.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL), Steve Ganon, alisema wamefarijika na ushindi huo.

“Kama familia ya SBL, tumefarijika sana kusikia habari hii kubwa inayoihusu bidhaa yetu, kitu kama hiki huwa hakitokei hivi hivi; tumekifanya kitokee... Kwa hiyo ninaipongeza timu nzima ya SBL kwa juhudi zao za kujenga imani kwa watumiaji.”

Bia ya Kibo Gold ilizinduliwa miaka 15 iliyopita chini ya Kibo Breweries. Hata hivyo haikudumu muda mrefu sokoni kutokana na kufungwa kwa Kampuni ya Kibo Breweries.

Nembo hiyo ilichukuliwa na Serengeti Breweries Ltd na kuzinduliwa upya Juni mwaka juzi katika kiwanda cha SBL kilichopo Moshi Brewery ambako ndiko huzalishwa na kusambazwa sehemu kubwa ya Kaskazini mwa Tanzania katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Manyara.

Agosti mwaka jana, Kibo Gold ilibadilishwa na kuwekwa katika chupa yenye shingo ndefu maarufu kama ‘mwanamke nyonga’ ili kwenda na wakati na matakwa ya soko la kisasa.

MCHICHA ni aina nyingine za ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi