loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kifo cha mjamzito chazua tafrani Sumbawanga

Wananchi walidai gari hilo lililotolewa kama msaada na Shirika lisilo la Kiserikali la Africare kwa kituo hicho, lilichelewa kufika na hivyo kusababisha kifo cha mwanamke huyo aliyekuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Mtowisa A.

Baada ya kifo cha Mwalimu Lea Mgaya juzi, inadaiwa wakazi wa eneo hilo, walishambulia kwa mawe na kuvunja moja ya vioo vya gari baada ya kushindwa kumnyang’anya funguo dereva wa gari hiyo aliyefika kituoni kumchukua mjamzito huyo anayedaiwa kupoteza damu nyingi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Ofisa Tarafa ya Mtowisa, Peter Masindi alisema awali, mwalimu huyo alipele kwa kituoni hapo asubuhi akiwa katika hali uchungu wa kujifungua lakini baadaye ilionekana anahitaji kupewa rufaa kwenda Hospitali ya Mkoa wa Rukwa, mjini Sumbawanga.

Masindi alisema ililazimu adhuhuri kupiga simu Ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya kuomba msaada wa gari lakini gari ilichelewa kufika kutokana na kukwama njiani ambako kulitokana na hali ya mvua iliyosababisha magari kushindwa kupita hadi saa 1 usiku lilipofika eneo la tukio na kukuta mjamzito huyo akiwa amefariki.

Miongoni mwa waliozungumza na mwandishi, walidai hasira zao zilitokana na kukerwa na kitendo cha gari hilo lililotolewa kwa ajili ya kituo chao, kutokukaa kituoni hapo.

“Hasira za wananchi hao zilionekana baada ya kufika kwa dereva wa gari hiyo aliyefika huku akiliza king’ora, lakini alipokewa na vijana waliokuwa na mabango ndipo walipomsimamisha wakiwa wameweka magogo njiani,” alisema Mwaipungu.

Aliendelea kusema, “Walimtaka kuwapa funguo za gari lakini dereva huyo alifanikiwa kupita pembeni kukimbia na gari hilo huku wananchi hao wakilishambulia kwa mawe.”

Kwa mujibu wa wakazi hao, kumekuwapo matukio matatu mfululizo ya vifo vya wajawazito katika miezi miwili kutokana na kukosa msaada wa haraka wa gari kuwapeleka hospitali ya mkoa.

Inadaiwa usiku huo lilipita gari la Bohari ya Madawa (MSD) wakalikimbilia na kuanza kulishambulia wakidhani ni gari la halmashauri kabla ya dereva wake kusimama na kujitetea ndipo walipomwachia.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi