loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kigoda: Dhamira ya dhati itakomesha bidhaa hafifu

Kwa mujibu wake, pamoja na kujihakikishia dhamira hiyo na kutekeleza wajibu wake kama taasisi inayotegemewa kuhakikisha kuwa Watanzania hawauziwi bidhaa zisizo na viwango vya ubora vinavyo kubalika kitaifa na kimataifa.

Shirika hilo halina budi kujitathmini kuona ni wapi linahitaji kupaboresha, ikiwa ni pamoja na kuangalia namna inavyoweza kutatua baadhi ya changamoto zinazoendelea kulikabili.

Aidha, anazungumzia jamii na kusema kuwa ili iweze kuwa na dhana ya dhati ya kukomesha uwepo wa bidhaa na huduma zisizo na ubora stahili, inapaswa kuwa na elimu ya kutosha kuhusu viwango vya ubora, ili inapozikataa bidhaa na huduma zisizokidhi viwango hivyo, iwe na sababu ya kufanya hivyo.

Kutokana na maelezo ya Waziri Kigoda, bila ufahamu wa ipi ni bidhaa au huduma yenye kiwango sahihi, na ipi haina kiwango cha ubora kinachotakiwa, jamii itaendelea kuzitumia, hivyo kuongeza kasi ya uzalishwaji, usambazwaji na uuzwaji wake.

“Serikali inafahamu changamoto inayolikabili Shirika la Viwango Tanzania, katika vita yake dhidi ya bidhaa hafifu, zilizopo sokoni na zinazoendelea kuzalishwa, kuingizwa na kusambazwa katika masoko mbalimbali ya bidhaa na huduma nchini…” Waziri Kigoda anasema.

Anaongeza kuwa, Serikali inatambua pia ugumu unaolipata shirika hilo katika jitihada zake za kukomesha uwepo wa bidhaa hafifu sokoni, hivyo kuwa nalo bega kwa bega kuhakikisha linatimiza malengo yake kwa faida ya watanzania na watu wengine wanaotegemea soko la Tanzania.

“Matarajio ya watanzania yanaweza kufikiwa endapo watanzania wenyewe, shirika la viwango na jumuiya ya wafanyabiashara nchini, watashirikiana kwa dhati, kuhakikisha kinachoingizwa sokoni ndicho kinachofaa, kwa kuwa na ubora unaokidhi kiwango cha bidhaa au huduma husika, kilichopitishwa na TBS,” anasema.

Aidha, Waziri Kigoda anaongeza kuwa, Baraza la Wafanyakazi wa shirika hilo, nalo lina nafasi kubwa ya kuhakikisha kuwa malengo ya TBS yanafanikiwa kwa asilimia 100 kwa kuwa linawajibika kulisaidia shirika hilo kwa kutoa sura mpya ya muundo na mfumo wa utendaji.

“Likiwa ndio mwakilishi wa wafanyakazi, Baraza la wafanyakazi wa TBS linapaswa kutekeleza wajibu wake kwa kuzingatia weledi, umakini na kuweka mbele umaslahi ya shirika na taifa kwa ujumla,” anasema

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TBS, Profesa Cuthbert Mhilu anasema kuendelea kuwepo kwa bidhaa na huduma zisizo na viwango vinavyotakiwa, kwa kuzingatia sheria ya viwango ya shirika hilo kunatokana na baadhi ya wanajamii kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu suala zina la viwango.

Hata hivyo, shirika linakiri kuwa linafanya jitihada mbalimbali kuhakikisha elimu hiyo ya viwango vya ubora inamfikia kila mwana jamii nchini, ikiwa ni moja ya mikakati yake ya kufanikisha lengo la shirika hilo kuondoa bidhaa hafifu katika soko la Tanzania.

“Jamii yote ikishapata elimu na kuelewa mambo muhimu yahusuyo viwango vya ubora wa bidhaa, kwa kiwango kinachotakiwa, bidhaa zisizo na ubora zitakosa wanunuzi, hivyo kujiondoa sokoni”.

“Elimu ndogo ya viwango kwa baadhi ya wanajamii ni miongoni mwa changamoto zinazolikabili shirika hili, hivyo kulifanya liongeze jitihada katika kuhakikisha watu wote wanapata taarifa zake, hasa kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini, semina, vipeperushi na njia nyingine zinazoweza kusaidia kusambaza habari muhimu kuhusu viwango,” anasema.

Profesa Mhilu anaeleza jinsi mshikamano wa wafanyakazi na menejimenti ya shirika hilo inavyosaidia kuleta maendeleo na kusema, “Katika robo tatu za mwanzo za mwaka wa fedha, shirika limeweza kutayarisha viwango vipatavyo 112 sawa na asilimia 89.6 ya lengo la kutayarisha viwango 125”.

Anasema ni kwa kuendekeza utamaduni wa kushirikiana, TBS imeweza kuwa na mtazamo mmoja juu ya kutekeleza mambo makuu matano ambayo ni; kuchagiza uchumi wa nchi, kusimamia afya, usalama na ustawi wa watu, kusaidia kuwalinda walaji, kuchagiza biashara za ndani na nje ya nchi, na kusimamia ushirikiano wa kimataifa katika nyanja za viwango.

“Kwa pamoja, kupitia ushirikiano thabiti wa wafanyakazi menejimenti na jamii, tuna nia ya kuhakikisha kuwa, lengo kuu la Serikali kuhakikisha soko la Tanzania linakuwa na bidhaa zenye ubora wa kushindana katika soko la ndani na la kimataifa linatimia,” anaeleza.

Kutokana na maelezo yake, msisitizo unaowekwa na shirika kwa sasa ni wa ushirikiano na jamii ya watumiaji, wazalishaji na wafanyabiashara wengine, kwa sababu bila ushirikiano wao, shirika litachukua muda mrefu kufikia malengo yake ya kuimarisha soko la ndani kwa bidhaa bora pekee.

Anasema, panapokuwa na ushirikiano mzuri kati ya baraza la wafanyakazi na menejimenti ya shirika hilo, ushauri wa baraza kwa menejimenti, kuhusu masuala ya kisera na kiutendaji unakuwa ni wa kujenga, kama inavyoonekana sasa.

Kadhalika, anasema, panapokuwa na ushirikiano baina ya jamii tofauti nchini, na shirika kwa ujumla, maoni yenye nia ya kujenga hutolewa na kufanyiwa kazi na shirika kwa kadri inavyostahili.

TAMKO la Kimataifa Kuhusu Haki za Binadamu (UDHR 1948), Mkataba ...

foto
Mwandishi: Namsembaeli Mduma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi