loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kijana jitambue

Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuwa miongoni mwa wateule wanaovuta pumzi yake, naendelea kukandamiza kibara, maisha ndiyo haya, leo nipo, ya kesho anayafahamu mwenyewe.

Hongera kwa vijana wote mnaotimiza wajibu wenu popote mlipo, na mnaotumia juhudi na maarifa kufika mlikokusudia.

Endeleeni na moyo huohuo, tumieni vizuri siku za ujana wenu kwa sababu umri haurudi nyuma, na huwezi kuuzuia uzee, na kufa ni lazima.

Natambua vijana mna majukumu ya kikazi na kifamilia, timizeni wajibu wenu, itumieni leo kujenga msongo wa maisha yenu ya kesho ile siku ya siku usiseme ningejua!

Pamoja na yote hayo tunastahili kufurahi, mimi kila wakati najitahidi kadri ninavyoweza niwe na furaha na ikiwa ni lazima kuikosa huwa nakubali matokeo, ninaamini kwamba siwezi kulazimisha kufurahi, na ninaweza hata kucheka wakati sina furaha.

Naithamini sana furaha kwa sababu ninaamini ina nafasi yake katika maisha ya mwanadamu yeyote na sina wakati mwingine wa kufurahi zaidi ya leo.

Furaha ni muhimu kwa mwanadamu na sidhani kama nitapata fursa nyingine ya kufurahi baada ya kuiaga dunia hii yenye raha, karaha, changamoto, masumbuko, vibweka n.k.

Jitambue, jipe muda wa kufahamu nafsi yako inahitaji nini ili ifurahi, usiige, jitahidi kuwa wewe na usijali wengine wanafanya au kusema nini.

Kaa leo jiulize unahitaji nini ili ufurahi, jibu utakalopata lifanyie kazi. Kila mara huwa najiuliza, nahitaji kufanya nini ili nifurahi, na huwa nafanya ambacho moyo wangu unataka nikifanye popote, vyovyote na ikibidi huwa nawashirikisha wengine kwa kadri ninavyoweza.

Vijana wengi hawana furaha, si kosa lao, ni kwa sababu hawajitambui na hawajaona umuhimu wa kufanya hivyo. Kujitambua ni muhimu sana katika maisha.

Tafuta muda ujiulize wewe ni nani, kwa nini upo ulivyo, na nini kimekuwa kikwazo cha furaha yako. Mimi najitambua ndiyo maana nafanya yale ninayoyafanya ili kufurahi.

Ili ufurahi si lazima uwe tajiri, na siamini kama matajiri wote wana furaha. Unaweza kufurahi hata kama huna ajira au huna mwelekeo wa maisha, na kwa kifupi ni kwamba, unaweza kuzikosa starehe lakini ukawa na furaha, siku njema.

Waziri Mkuu Mstaafu, ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi