loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kikwete afanya uteuzi Mambo ya Ndani

Kamati ya Kuzuia Biashara Haramu ya Binadamu ilianzishwa chini ya Sheria ya Kuzuia Biashara Haramu ya Binadamu ya mwaka 2008 na kazi kubwa ya Kamati hii ni kuzuia na kudhibiti biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu.

Chimbuko la kutungwa kwa Sheria ya Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu ni Itifaki ya Kimataifa ya kuzuia, kupambana na kutoa adhabu kwa watekelezaji wa biashara ya usafirishaji haramu ya binadamu, hasa wanawake na watoto.

Tanzania imeridhia Makosa yanayovunja Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu ni pamoja na kupanga, kupangisha au kutumia nyumba au jengo kwa ajili ya biashara ya usafirishaji wa binadamu na kughushi hati za Serikali kwa madhumuni ya kukuza biashara ya binadamu.

Makosa mengine ni kujipatia pesa kwa kuwatumikisha kwa nguvu watu wazima au watoto wa kike au kiume katika kufanya kazi za ndani au biashara nyingine haramu kama ngono na usafirishaji na usambazaji wa dawa za kulevya, baada ya kuwalaghai au kuwachukua kwa nguvu kutoka katika makazi yao.

Adhabu kwa wanaotiwa hatiani kwa kuvunja Sheria hii ni kifungo kisichopungua mwaka mmoja (1) au kisichozidi miaka saba (7) au faini isiyopungua Sh milioni mbili (2) au kuzidi Sh milioni 50 au vyote kwa pamoja.

WASHEREHESHAJI katika matukio mbalimbali zikiwamo sherehe za harusi, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi