loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kikwete anguruma Umoja wa Mataifa

Rais Kikwete amesema hayo wakati akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) juzi jijini New York, Marekani.

Rais Kikwete alisema anatarajia majadiliano yatatoa nafasi kwa nchi kupanga mipango ya baadae kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

"Tutumie muda huu kuendeleza mafanikio na mafunzo kutoka nchi mbalimbali na pia tujifunze kutokana na changamoto za kushindwa kufikia Malengo ya Milenia, na kuzitumia kama viashiria vya ajenda ya Maendeleo baada ya Mwaka 2015," alisema Kikwete.

Rais ameiasa dunia kujadili ajenda ya Maendeleo baada ya mwaka 2015, pasipo kusahau malengo ya milenia ambayo hayajakamilika na kuyaweka vizuri katika ajenda mpya.

Pamoja na umuhimu wa MDGs, Rais Kikwete amezungumzia suala la tabianchi na kuzitaka nchi zote duniani kukusanya nguvu katika suala hili ili kuiokoa dunia kutokana na majanga ya tabia nchi.

Masuala mengine ambayo Rais alizungumzia ni Mageuzi katika UN, ambapo alisema yanasuasua na hali ya usalama duniani ambapo unatishiwa na ugaidi.

Pia alizungumzia uhasama baina ya Israel na Palestina, ambao alisema umedumu kwa muda mrefu hivyo kuutaka Umoja wa Mataifa kutafutia suluhu ya kudumu.

Masuala mengine ni Sahara Magharibi ambalo pia limedumu kwa muda mrefu bila ufumbuzi, vikwazo kwa nchi ya Cuba ambavyo navyo vimekuwepo kwa muda mrefu na kuutaka Umoja wa Mataifa kutafuta utatuzi wa kudumu.

Rais Kikwete pia amezungumzia ugonjwa wa ebola ambao tayari umeua watu wapatao 2,400 na haujadhibitiwa.

"Juhudi za pamoja zinahitajika kwani ndiyo njia sahihi, naamini kuna teknolojia na rasilimali za utaalamu na fedha ambavyo kwa pamoja, tunaweza kushinda tishio la ugonjwa huu," amesema.

Rais amezitaka juhudi zaidi zifanyike katika kuudhibiti, kwa kuwa ugonjwa huu ni hatari na unaweza kuwa janga la dunia.

RAIS John Magufuli amewataka wasaidizi wake ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, New York

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi