loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kikwete apongeza wasomi wanaolima, kuwasaidia

“Ni kazi gani itakayokupa Sh milioni 23 kwa mwaka labda uwe na mshahara mkubwa sana,” alisema.

Pamoja na kuwapa pongezi vijana hao, pia aliahidi kukipatia kikundi hicho msaada wa kuchimbiwa kisima kirefu cha maji na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi na kuwa na masoko ya uhakika wa bidhaa zao.

Alisema kuwepo kwa kikundi hicho ni utekelezaji wa sera ya serikali iliyopo madarakani, ambayo inatoa fursa ya maisha bora kwa kila Mtanzania kwa kuangalia fursa zilizopo.

Alisema hayo juzi wakati akihutubia wananchi wa Tarafa ya Mundemu Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, ambapo pia alizindua Kituo cha Rasilimali za Kilimo na Mifugo. Alisema kitendo cha vijana hao wasomi ni cha kupigiwa mfano.

Aliwataka vijana kutopuuza kilimo, kwani kina uwezo mkubwa wa kuwainua kiuchumi.

“Unaweza kwenda kijijini ukakutana na mtu unamuuliza anafanya kazi gani, anasema hana kazi ila analima tu, bila kujua kuwa kilimo nacho ni kazi ya maana sana,” alisema.

Alisema huu ni wakati wa kila moja, kubadili mtazamo juu ya kilimo, kwani wengi wanatamani kuajiriwa, bila kufahamu kuna fursa kubwa zaidi katika kujiajiri.

Aidha, alisema serikali iliyopo madarakani, imetekeleza kwa kiasi kikubwa kwa vitendo ahadi zake; na miradi mingi ya maendeleo imewafikia wananchi. Rais Kikwete alisema asingependa kuona CCM ikisutwa, kwa kushindwa kuwaletea maendeleo wananchi wake.

“Nisingependa Chama Cha Mapinduzi kisutwe kwa kushindwa kuwaletea maendeleo watu wake, lakini wa kusema na kuzoza wapo tu; na kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala,” alisema

Akizungumzia elimu, alisema shabaha ya serikali ni kuongeza ubora wa elimu na kuboresha miundombinu katika shule za msingi na sekondari. Alisema mkazo mkubwa sasa, unaelekezwa kupatikana kwa walimu wengi wa sayansi.

Alisema sasa kuna upungufu wa walimu wa sayansi 23,500 na uwezo wa vyuo kutoa walimu wa sayansi ni 2500 tu kwa mwaka, jambo ambalo linahitaji mkazo zaidi ili kupunuza pengo lililopo.

Alitaja shabaha nyingine ya serikali kuwa ni kupunguza tatizo la vitabu.

“Tunataka kila mtoto kuwa na kitabu chake, hilo halitatushinda,” alisema. Alisema sasa kila shule ya sekondari inatakiwa kuwa na maabara ya sayansi ili kuwe na wataalam wengi wa sayansi na walimu wengi watatoka hapo.

RAIS John Pombe Magufuli anaongoza kwenye ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi