loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kikwete apongezwa kwa dhamira ya kutokomeza umasikini

Pongezi hizo zilitolewa juzi na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, Robert Kamoga alipokuwa akihitimisha warsha ya kujenga uelewa wa wadau kuhusu mpango wa kunusuru kaya masikini unaoasisiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) awamu ya tatu.

Alisema uongozi wa Rais Jakaya Kikwete umeimarisha zaidi dhamira ya nchi kupunguza umasikini kupitia mikakati yake mbalimbali na kuboresha upatikanaji wa huduma za kijamii ambazo ni pamoja na elimu, afya na maji kwa ushirikiano mkubwa na wananchi.

“Nachukua nafasi hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete kwa uongozi wake ambao umeonesha dhamira ya dhati ya nchi hii kupunguza umasikini wa wananchi sambamba na kuboresha huduma za kijamii,” alisema Kamoga.

Alisema kitendo cha Rais Kikwete kuzindua Mpango maalumu wa Kunusuru Kaya Maskini Agosti 15, 2012 kule Dodoma na utekelezaji wake kuanza mara moja mwezi Februari 2013 unaonesha ni kwa namna gani amedhamiria kutokomeza umasikini katika kaya.

Kamoga alibainisha kuwa madhumuni ya mpango huu wa awamu ya tatu ya TASAF ni kuwezesha kaya maskini kuongeza kipato, fursa na uwezo wa kugharamia mahitaji yao muhimu na familia zao mpango ambao utatekelezwa kwa awamu katika kipindi cha miaka 10.

Aidha aliwakumbusha washiriki wa kongamano hilo kuwa TASAF ni chombo cha serikali kilichopewa jukumu la kuwezesha kufikia azma ya serikali ya kupunguza umaskini kama ilivyoainishwa katika awamu ya pili ya MKUKUTA kwa kutumia dhana ya ushirikishwaji jamii.

Aliongeza kuwa tangu nchi yetu ipate uhuru miaka 50 iliyopita, serikali imekuwa ikipambana na maadui watatu ambao ni umaskini, ujinga na maradhi, lengo likiwa kumwondolea mwananchi kero na vikwazo mbalimbali vya kimaendeleo.

Kamoga alieleza kuwa serikali kwa kutambua kwamba umaskini bado ni mkubwa miongoni mwa jamii hasa kule vijijini, ndio maana imeandaa Mpango huu wa Kunusuru Kaya Maskini ili kufikia malengo yake iliyoazimia katika Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA ) awamu ya pili.

Awali akizungumza katika warsha hiyo Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Peter Luanda alisema mpango huo wa kunusuru kaya maskini umelenga kuzinufaisha kaya masikini zilizo katika hali duni kule vijijini na katika mitaa mbalimbali hususani watoto wenye umri chini ya miaka 5 na wanaosoma shule na akina mama wajawazito.

Alisema kaya hizo zitanufaika kwa kupewa ruzuku za aina mbili moja ni ruzuku ya msingi itakayotolewa kwa kaya maskini iliyomo kwenye mpango huo na ruzuku ya pili walengwa ni wale wanaotakiwa kutimiza masharti ya elimu na afya ili waweze kupatiwa huduma za elimu na afya bure.

Akizungumza baada ya warsha hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya Sikonge, Shadrack Mhagama alipongeza ujio wa mpango huo wa TASAF wa kunusuru kaya maskini na kuongeza kuwa utasaidia kuboresha maisha ya wananchi wake kwani wengi wao wamekuwa wakishindwa kuchangia hata shughuli za maendeleo kutokana na kuwa na hali duni.

Rais John Magufuli amesema Manispaa ya Ilala imepandishwa ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Sikonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi