loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kikwete ashangaa viongozi wanaoua, kutesa raia

Aidha Rais Kikwete pia amesema kuwa Mpango wa Nchi za Afrika Kujithamini Kuhusu Utawala Bora (APRM) ni mfumo mzuri sana ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kiwango cha udikteta katika Bara la Afrika.

Alikuwa anajibu swali katika mazungumzo na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Jamhuri ya Watu wa China kwenye siku yake ya pili ya ziara rasmi ya Kiserikali ya siku sita kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping.

Akijibu swali la Balozi Sola Onadipe, Naibu Balozi wa Nigeria katika China, Rais Kikwete alisema mfumo wa APRM umekuwa wa manufaa makubwa kwa Bara la Afrika na hasa kwenye mifumo ya Utawala Bora wa nchi za Afrika.

“APRM ni chombo murua sana. Kimesaidia sana kuboresha mifumo yetu ya Utawala Bora, hata kama bado wapo watu wanaosema kuwa APRM na falsafa yake ni jambo la Wazungu jambo ambalo siyo la kweli kwa kutilia maanani faida za mfumo huu wa kujithamini wenyewe,” alisema Rais Kikwete.

“Hivi tunahitaji Wazungu kuja kutufundisha kuwa ni jambo baya kuua raia wako? Unahitaji Mzungu aje kukuambia kuwa ni jambo baya kufanya ukatili na unyama kwa wananchi wako?...”

Rais Kikwete alisema mageuzi na mabadiliko ya kidemokrasia katika nchi za Afrika ni jambo zuri na ni jambo la lazima na kwamba viongozi wa Bara hilo lazima waendelee kukumbatia, kulea na kuendelea kujenga demokrasia.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Beijing

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi