loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kikwete: Licha ya ebola, Afrika iko salama

Aidha, Rais Kikwete amesema Tanzania imetuma madaktari watano kwenda Afrika Magharibi kusaidia kukabiliana na ugonjwa wa ebola ambao unaendelea kuua maelfu ya watu katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.

Mpaka sasa watu zaidi ya 4,000 wamepoteza maisha kwa ugonjwa huo katika nchi hizo.

Rais Kikwete aliyasema hayo juzi kwenye Nyumba ya Kufikia Wageni ya Serikali ya Diaoyutai mjini Benjing, wakati alipokutana na kuzungumza na mabalozi wa Afrika wanaoziwakilisha nchi zao nchini China ikiwa ni shughuli yake ya kwanza ya ziara yake rasmi ya kiserikali nchini humo.

Katika mkutano wake na mabalozi hao wa Afrika, alipata nafasi ya kuwaeleza hali ya kisiasa, kiuchumi na kiusalama Barani Afrika hasa katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Libya, Sudan Kusini na Somalia na tishio la ugaidi wa makundi mbalimbali katika nchi za Afrika.

“Lakini habari kubwa katika Afrika kwa sasa ni ugonjwa wa ebola. Bara la Afrika linabaguliwa sasa kwa sababu ya ugonjwa huo. Watu wanafuta mipango yao kutembelea Bara letu, watalii wanapungua. Kwetu sisi ugonjwa huu ni tishio kubwa kwa maisha ya watu wetu lakini ni tishio kubwa kiuchumi,” Rais Kikwete amewaambia mabalozi hao na kuongeza:

“Sasa kwa sababu ugonjwa wa ebola unaongeza kubaguliwa kwa Bara la Afrika, ni wajibu wenu nyie wawakilishi wetu, mabalozi wetu kutusemea. Elezeni habari njema na nzuri za Afrika" alisema.

Kuhusu mchango wa Tanzania katika kukabiliana na ugonjwa wa ebola, Rais Kikwete alisema kuwa Tanzania imetuma madaktari wake watano katika nchi zinazokabiliwa na ugonjwa huo kwa sasa kuongeza nguvu za kukabiliana na ebola.

“Nchi za Afrika zinahitaji sana mshikamano na ushirikiano kwa sasa kukabiliana na ugonjwa huo hatari sana.”

RAIS John Magufuli amewataka wasaidizi wake ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Beijing

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi