loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kila la heri Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Tunapenda kuwatakia kila la heri wenzetu waliojaliwa kufunga msimu huu kuwa na uvumilivu na upendo katiki kipindi chote cha mfungo hadi hapo utakafikia tamati.

Tunajua kwamba nchi yetu hivi sasa inapitia katika kipindi kikugumu cha mpito kwa msauala mazima ya kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kijamii hivyo kunahitajika umakini wa aina yake katika kuyafikia malengo hayo ya kila taifa makini duniani.

Kubwa tunalotaka kuwakumbusha viongozi wetu katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni kuiombea nchi yetu iweze kuendelea kuwa kisiwa cha amani na upendo kama walivyoicha wasisi wa Taifu hili, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume.

Sote tunakumbuka kwamba wasisi hao walituongoza watanzania kwa misingi ya haki, upendo na mshikamano na pia kutuelekeza kwamba Tanzania isingeweza kuwa nchi huru kama baadhi ya nchi za bara hili la Afrika zingendelea kukaliwa na wakoloni, jambo ambalo tulilikataa kwa vitendo kwa kusadia ndugu zetu katika nchi nyingine walikuwa wanadai uhuru wao hadi kufanikiwa.

Hii ndiyo nchi iliyoachwa na waasisi hao ikiwa na umoja, mshikamano, upendo na kupiga vita ubaguzi wowote ukiwemo wa rangi, ukabila,dini na jinsia.

Kutokana na malezi hayo Tanzania imekuwa inaendelea kuwa kisima cha amani kwa bara letu la Afrika na duniani kwa ujumla wake.

Ni nani asiyefahamu kwamba Tanzania tangu nyakati za awali za kupata uhuru wake imekuwa ni kimbilio la wananchi wengi walikuwa wanakumbwa na madhila mbalimbali na mateso katika nchi zao?

Ni nani ambaye hujui kwamba makao makuu ya kamati ya Ukombozi Barani Afrika yalikuwa hapa nchini na kutoka hapa ndipo wapigania uhuru katika nchi mbalimbali walipata mafunzo ya kuwang'oa wakoloni katika nchi zao hadi kupata uhuru?.

Tanzania imejengwa kudumisha amani siyo kwa kubahatisha bali kwa makusdi na kwa matendo ambayo watanzania wote wakiwemo viongozi wa serikali, dini, vyama vya kirai na kila mmoja wetu asithubuti kuichezea na iwapo atatokea mtu wa aina hiyo tumbezi sote kwa umoja wetu.

Tuna imani kwamba kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Watanzania wote na wenzetu wanaojaaliwa kufunga tuiombee amani yetu hususani ni tuweze kuvuka salama wakati Bunge letu la Kutunga Katiba Mpya litakaporejea Agosti mwaka huu mjini Dodoma ili waweze kukamilisha kwa amani, usalama na maridhino ya kazi tuliyowatuma ya kutuletea katiba mpya ya nchi yetu.

Tuwaombee katika kipindi hiki kwa dhati wajumbe wetu wanaotuwakilisha katika Bunge hilo Maalum la Katibu waweze kufikia muafaka wa kutuletea Katiba Mpya tunayoisubiri kwa hamu sisi sote ili kuendelea na hatua itakayofuata.Mungu ibariki Tanzania.

FUKUTO la Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani linazidi ...

foto
Mwandishi: mhariri

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi