loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kila mtumishi atakiwa kuwa na akaunti

Aidha imetaka watumishi wote wa umma walipwe mishahara moja kwa moja kupitia akaunti zao sahihi za benki ambazo zitatumika kupitishia mishahara yao. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Alisema kila mtumishi afungue akaunti benki ikiwa ni hatua ya kudhibiti mishahara hewa na kuweka uwazi.

“Waajiri watakaoshindwa kutoa ‘Payroll’ watasababisha watumishi wanaowaongoza kushindwa kupata mishahara yao kwa mwezi husika jambo ambalo si nia ya Serikali,” alisisitiza Nchemba.

Alisema Julai walipolipa kwa kutumia akaunti waligundua kwamba wafanyakazi zaidi ya 14,000 walikuwa wanaeleaelea na ni hewa na wafanyakazi zaidi ya 1,900 waliokuwa wanapokea fedha madirishani walipotea ambapo kati ya Sh bilioni 40 hadi 50 zilipona kwa sababu hazikupelekwa.

“Mishahara ya watumishi wote wa Serikali, wakala na taasisi za umma italipwa moja kwa moja kupitia akaunti zao za benki,” alisema.

Katika kufanikisha hilo, Nchemba aliagiza waajiri wote wa sekta ya umma kuwa na namba za akaunti ya benki za watumishi wote waliochini ya fungu husika ambazo zina taarifa sahihi na wakizingatia mfumo sahihi wa taarifa za kiutumishi.

Alionya kuwa mtumishi asiye na akaunti benki asilipwe mshahara wake dirishani. Alihimiza waajiri kusisitiza watumishi walio chini yao kufungua akaunti sahihi ya benki kwenye mfumo utakaotumika kulipa mshahara husika kupitia orodha ya malipo ya mshahara inayotolewa na Hazina.

“Kwa mujibu wa Waziri, utaratibu huo wa kulipa mishahara utakuwa endelevu na umedhihirisha kuwa na tija kwa matumizi ya fedha za umma kwa kuonesha mafanikio ambayo kwa Julai na Agosti mwaka huu, hakuna mtumishi, Wakala za Serikali wala taasisi waliolalamika kukosa mshahara.

RAIS John Magufuli amewataka wasaidizi wake ...

foto
Mwandishi: Hellen Mlacky

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi