loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kinana aonya uzalishaji gesi dampo la Mtoni

Kinana aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati alipotembelea mradi huo ikiwa ni siku yake ya pili ya ziara yake mkoani humo ya kukagua utekelezaji wa ilani na uhai wa chama hicho cha CCM.

Alisema pamoja na kwamba wakazi wa eneo wanautegemea zaidi mradi huo ukweli ni kwamba ulianzishwa kuendana na mtindo wa kidunia ambapo wajanja wachache walitumia fursa hiyo na kukimbilia Tanzania na kuwekeza baada ya kunufaika wakautelekeza.

“Mradi huu ulitokana na kampeni za utunzaji wa mazingira zilizoanzishwa na Umoja wa nchi za Ulaya na UN, hasa baada ya kuwepo kwa mabadiliko ya tabia nchi, katika kampeni hizo kulikuwa na mfuko maalum wa mazingira ambapo mtu au kampuni itakayoweza kusafisha mazingira katika eneo lolote kwa uniti moja, alikuwa akilipwa euro 20 sawa na Sh 50,000,” alisema Kinana.

Hata hivyo, alisema pamoja na muwekezaji huyo kutekeleza mradi huo, bado wapo wawekezaji wengine wameonesha nia ya kuuendeleza.

“Hili sasa namuachia Mkuu wa Mkoa alishughulikie anaweza kuwaangalia wawekezaji hawa, lakini sasa hakikisheni wanapewa mradi huu kwa masharti na taratibu za kitanzania na manufaa ya Watanzania.”

Alisema imekuwa kawaida kwa mataifa ya nje kwenda na mitindo mbalimbali ya miradi kwa ajili ya kujinufaisha wao.

“Huu mradi ulikuwa katika mtindo wa mazingira, ulikuwepo mtindo wa wanawake juzi ulikuwepo wa kutetea maalbino nao unaelekea kuisha, miradi hii tuwe nayo makini sana.”

Pamoja na hayo Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu, amemuomba Katibu Mkuu huyo kusaidia kuuhamisha mradi huo kutoka Halmashauri ya Jiji na kuupeleka Manispaa ya Temeke, ili kuunusuru usiuzwe kwa bei ya kutupa au kufa.

Mtemvu alisema tangu kutelekezwa kwa mradi huo na muwekezaji ambaye ni Muitaliano mwaka 2007, haujaendelezwa na una dalili zote za kufa kutokana na hali ya kifedha ya Halmashauri ya Jiji ilivyo.

“Mheshimiwa Katibu sisi tunaomba mradi huu uje Manispaa ya Temeke tutatafuta wafadhili uendelezwe, kwa sasa uko chini ya Jiji na sote tunawajua hali zao, wanaweza wakauuza kama walivyouza miradi mingine kama vile UDA,” alisema Mtemvu.

Alisema Halmashauri ya Jiji imekuwa na kawaida ya kuuza au kuacha miradi ife pindi inaposhindwa kuiendeleza. “Sisi tunajua iwapo mradi huu tusipoingilia kati utauzwa au kufa wakati unafaida kwa wananchi, Jiji waliuza UDA kwa Sh milioni 250 ambazo hata sisi wabunge tungeweza kuzichanga tukainunua,” alisema.

Awali akiwasilisha taarifa ya kiwanda hicho cha gesi inayozalishwa kwa kutumia takataka, Meneja Mradi Richard Matari, alisema mradi huo ulijengwa kwa gharama ya Sh bilioni mbili tangu mwaka 2003, kupitia mradi wa Umoja wa Mataifa wa kutunza mazingira.

Hata hivyo, alisema mradi huo ulifanya kazi kwa muda mchache na baadaye mwekezaji aliutelekeza kwa kuondoka bila kubadilisha jina la akaunti ya kiwanda hicho na tangu kipindi hicho Halmashauri ya Jiji ilishindwa kuuendeleza kutokana na ukosefu wa fedha.

WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi