loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Kinondoni mabingwa ARS 2014

Fainali hiyo ilichezwa kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam juzi na ilitanguliwa na shamrashamra za maandamano na halaiki.

Ilikuwa yenye upinzani mkali na baada ya kosakosa za hapa na pale Kinondoni walipata bao katika dakika ya 31 lililofungwa na Kassim Kitwana kwa shuti kali la mbali lililomshinda kipa wa Ilala, Salum Siasa.

Bao hilo lilibadili kasi ya mchezo huku Ilala wakitafuta la kusawazisha na juhudi zao zilizaa matunda katika dakika ya 40 baada ya kutokea piga nikupige golini mwa Kinondoni na mchezaji hatari Juma Yusufu kufunga kwa shuti la karibu.

Kipindi cha pili kilianza kwa kushambuliana kwa zamu, lakini hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao la kuongoza hadi dakika ya mwisho.

Ndipo refa akaamua kumaliza ubishi kwa penalti. Katika penalti tano, Kinondoni walifunga kupitia kwa Abdul Malangali, Milaji Gwangaya, Omri Rashid na Abubakari Nuru wakati Kassim Kitwana alipaisha.

Waliofunga kwa Ilala ni Abdul Bitebo na Rashid Mohamed wakati Maisala Adam na nahodha Shaban Zuberi walikosa.

Akifunga fainali hizo za taifa za Airtel Rising Stars, mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante ole Gabriel kwa niaba ya Naibu Waziri Juma Nkamia, aliipongeza Kampuni ya Airtel kwa kujitokeza kusaidia maendeleo ya soka nchini.

Alitoa mwito kwa vijana kuzingatia nidhamu katika michezo na kujituma ili kupata mafanikio na kusema kuwa katika dunia ya leo, soka ni chanzo cha ajira kwa vijana wengi. Pia alisema kuwa kufanikiwa kwao kutaiwezesha Tanzania kufahamika zaidi kimataifa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso alisisitiza nia thabiti ya kampuni yake kuendelea kudhamini mashindano ya vijana ya Airtel Rising Stars.

RUVU Shooting, Kagera Sugar na Gwambina ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi