loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

‘Kipanya’ chaua watu 10

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 6:00 mchana imehusisha gari aina ya Toyota Hiace lililokuwa likitokea Jijini Mbeya na Fuso lililokuwa likitokea katika kituo cha mafuta na kuingia barabara kuu ya kutoka Mbeya kwenda Tunduma.

Akizungumzia ajali hiyo, Muuguzi Mkuu wa Hospitali teule ya wilaya ya Mbeya, Sikitu Mbilinyi alisema kuwa wamepokea maiti 10 wakiwemo wanawake wanne, wanaume wanne na watoto wawili.

Alisema katika majeruhi wanane waliopokelewa hospitalini hapo, watano ni wanaume na watatu ni wanawake na kwamba madaktari baada ya kubaini hali za majeruhi hao kuwa mbaya walishauri wapelekwe katika hospitali ya rufaa Mbeya .Tayari majeruhi watatu akiwemo mwanamke mmoja wamehamishiwa katika hospitali hiyo.

Aliwataja waliokufa katika ajali hiyo ambao wametambuliwa na ndugu zao kuwa ni pamoja na Mariam Mashambwe na mtoto wake Hamis Chaula, Rebeca Keneth, Petro mgogo, Haruna Jamison na Martin Mwasolikoto.

Aliwataja majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo na kulazwa kuwa ni pamoja na kondakta wa Hiace, Justin Chaula(28)mkazi wa Mabatini, kondakta wa lori Joseph Stephano (22) mkazi wa Mbalizi , aliyekuwa abiria wa roli Ziona Goa (20), Newton Patrick na dereva wa lori, Amoni Mwakoko.

Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo, Ziona Goa alisema kuwa Hiace waliyokuwa wamepanda ilikuwa na hitilafu katika breki na kusababisha gari kwenda kwa mwendo wa kasi na dereva kushindwa kulidhibiti na kuligonga lori ambalo tayari lilikuwa limeingia barabarani.

“Tulimsikia dereva akisema breki hazifanyi kazi huku gari likiwa kwenye mwendo kasi na ghafla mbele yetu kukawa na lori limekwisha ingia barabarani na tukaligonga ubavuni,” alisema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.

foto
Mwandishi: Merali Chawe, Mbeya

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi