loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kipingu aandaa bonanza la michezo

Bonanza hilo linaandaliwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania Iddi Kipingu kwa kushirikiana na mke wake Zuwena Kipingu.

Akizungumza na 'Habarileo' jana, Mkurugenzi wa mashindano wa klabu hiyo Zuwena Kipingu alisema bonanza hilo litahusisha timu za Mkoa wa Dar es Salaam na wachezaji wakongwe ambapo watashiriki michezo ya soka, netiboli, kuvuta kamba, ngumi, karate na mbio fupi.

“Ni bonanza ambalo limelenga katika kuhamasisha watu kupenda michezo na kujihusisha na mazoezi, wasiwe wanakaa tu ofisini bali wafanye mazoezi ili kuchangamsha mwili,” alisema.

Kipingu alisema bonanza hilo litadhaminiwa na Pepsi, Kampuni ya simu ya Airtel na bado anaendelea kufanya mazungumzo na baadhi ya kampuni na mashirikika mbalimbali zikiwemo NSSF, Bank ya Equit na Startimes na wakati huo akihimiza wengine kuwaunga mkono ili kufanikisha.

Alitaja baadhi ya timu zilizothibitisha kushiriki kuwa ni benki ya CRDB, NMB, Airtel, Wizara ya Mambo ya Ndani na Pepsi. Kwa mujibu wa Kipingu, bonanza hilo litapambwa na burudani kutoka kwa baadhi ya wasanii wa kizazi kipya, ngoma na ngumi.

Kipingu alisema hilo litakuwa ni bonanza la kwanza la aina yake ambapo litakuwa likifanyika kila mwaka tarehe hiyo na kuongeza kuwa lingine litafanyika jijini Mbeya Machi.

KLABU ya Simba  imetambulisha  mashindano mapya ya Super  Cup, ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi