loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Kisukari bado tishio nchini - Kebwe

Aidha, imesema endapo mtu atatambulika kuwa ana ugonjwa huo, atumie huduma za afya kulingana na ushauri wa atakaopewa na wataalamu wa afya.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe jana alipokuwa anatoa tamko kuhusu Siku ya Kisukari Duniani, itakayoadhimishwa Novemba 14, mwaka huu duniani kote yenye kaulimbiu “Ulaji unaofaa, huanza na mlo wa asubuhi”.

Alisema Siku ya Kisukari Duniani ilianzishwa baada ya kuona ugonjwa huo unaongezeka kwa kasi duniani.

Alisema Tanzania kama nchi nyingine duniani, huadhimisha siku hiyo kwa kushirikiana na Chama cha Ugonjwa wa Kisukari Tanzania kwa kutoa elimu ya umuhimu wa kuzuia na kujikinga na madhara mbalimbali yatokanayo na ugonjwa huu.

“Ugonjwa wa kisukari ni hali ambayo hutokea wakati sukari katika damu inapokuwa nyingi kupita kiwango cha kawaida kwa muda mrefu,” aliongeza Dk Kebwe.

Alibainisha kuwa asilimia 80 ya wagonjwa wa kisukari duniani, wanaishi katika nchi zinazoendelea, ikiwemo Tanzania. Alisema tafiti zinaonesha mwaka 2007 kulikuwa na wagonjwa milioni 246 duniani barani Afrika, mwaka 2012 wagonjwa milioni 371, mwaka 2013 wagonjwa milioni 382 na mwaka 2013 kulikuwa na wagonjwa milioni 19.8.

Kwa upande wa Tanzania, alisema utafiti uliofanyika mwaka 2012 na kuhusisha wilaya 50, ulionesha kuwa asilimia 9.1 ya Watanzania wenye umri wa miaka 25 na kuendelea wana ugonjwa wa kisukari.

Dk Kebwe alisema takwimu za watoto wenye kisukari mwaka huu ni kati ya asilimia 15 mpaka 20 ya wagonjwa wa kisukari ambao wanatibiwa kwenye kliniki nchini.

Alisema Tanzania inaungana na mataifa yote duniani, kutekeleza azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 2011 la kuhakikisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanapungua kwa asilimia 25 ifikapo mwaka 2025.

foto
Mwandishi: Beatrice Lyimo wa Maelezo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi