loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kituo kuwapa mikopo vijana kwa riba nafuu

Akizungumza jana jijini hapa wakati akielimisha vijana umuhimu wa kujiunga katika vikundi, Mkurugenzi wa kituo hicho, Victor Tesha alisema kwa kufanya hivyo, kutawaondoa vijana katika lindi la umasikini na kupunguza mzigo kwa Serikali.

Alisema kuwa mikopo hiyo itatolewa awamu ya kwanza Desemba mwaka huu kwa mfumo wa vifaa badala ya pesa. Alisema mikopo hiyo itatolewa kwa vijana wenye ujuzi, ambao watakusanyika na kujipanga kuanzisha mradi kwa malengo waliojiwekea.

Aidha kwa wasio na ujuzi wao watatakiwa kujikusanya sio pungufu ya kumi na wanne na malengo yanayofanana na kutafuta wataalamu wa biashara ili waweze kushauriwa kama kuna ulazima.

Tesha alisema vijana nchini ni waathirika wa ajira na kwa mujibu wa takwimu za sensa ya mwaka 2012 inaonesha vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 35 wanafikia asilimia 61.17 kati ya watu wote.

Alisema kikubwa cha kuzingatia kwa vijana wote ni kujisajili baada ya kujikusanya na watapatiwa mikopo ndani na nje ya nchi na riba yake itakuwa asilimia tano tu.

Naye mmoja wa vijana waliopatiwa mafunzo hayo, Elly Balton alisema fursa hiyo ni nzuri kwa vijana na wanapaswa kuchangamkia, sababu inalenga kumsaidia kijana kwa dhati, kuliko kumpatia pesa.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Arusha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi