loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Klabu 102 za michezo zapewa vifaa Ruangwa

Majaliwa ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa (Tamisemi), aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa kilele za sherehe za kutimiza miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizofanyika katika Kata ya Likunja wilayani humo.

Katika sherehe hizo, Mbunge huyo alizipatia timu za soka za Uhuru City na Mbagala City jezi seti moja kila timu na mpira mmoja, na kisha zilichuana ikiwa ni kusherehekea CCM kutimiza miaka 37.

Uhuru City iliibuka mshindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbagala City. Naibu Waziri Majaliwa pia ameviwezesha vikundi mbalimbali vya ngoma katika wilaya hiyo ambavyo vinajipatia fedha kwa ajili ya kazi ya sanaa na kujikwamua kiuchumi.

Sherehe hizo zilienda sambamba na maandamano ya wanachama wa CCM na kupambwa na burudani ya ngoma za asili, kwaya na muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali kikiwemo kikundi cha Wanapakaya kutoka wilayani Kilwa na msanii Dogo Doto.

TIMU ya Ruvu Shooting imeboresha kikosi ...

foto
Mwandishi: Anna Nkinda, Maelezo, aliyekuwa Ruangwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi