loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Klabu zibadilike kifikra

Stars sasa ina kibarua cha kutafuta ushindi katika mechi ya marudiano mjini Maputo, Agosti 3, mwaka huu ili kufuzu kwa hatua ya mwisho ya mchujo ambayo ni makundi kuwania nafasi 14 za kwenda Morocco.

Mengi yamesemwa baada ya matokeo hayo, lakini tunachokiona sisi ni kwamba klabu za Tanzania hazina budi kwenda mbali kifikra kama zinataka Stars ifanye vizuri katika mashindano mbalimbali.

Ndio lazima ziende mbali kimtazamo na kuufanyia kazi ushauri wa kitaaluma juu ya namna ya kuuendesha mchezo wa soka na hatimaye timu yetu ya taifa kufanya vizuri.

Kama hali itaendelea hivi katika mfumo wa sasa, tusitarajie maajabu kuwa siku moja timu yetu inaweza kufuzu kwa fainali nini za Kombe la Dunia, bali hata za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani(Chan) na fainali za Mataifa ya Afrika zinazoshirikisha wachezaji wa kulipwa (Afcon).

Tuna safari ndefu sana, lakini kikubwa ni kuwa na majibu rahisi kwa maswali magumu yanayoukabili mchezo wetu. Kila mtaalamu anayekuja nchini ukimuuliza Tanzania ifanye nini ili ipate maendeleo ya kweli katika soka lake, anakupa majibu yale yale tu ya kwamba kuendesha mchezo wa soka kwa weledi mkubwa tukianzia na timu za vijana za ngazi zote.

Kikubwa hapa ni kuandaa misingi ya mchezo wa soka kuanzia miundombinu yake kwa maana ya viwanja, makocha, waamuzi, watawala wa mchezo wenyewe, mashabiki mpaka kufikia kwa wachezaji wenyewe; hapa weledi mkubwa unatakiwa.

Yakishindikana haya hali itakuwa ile ile kama tuliyoiona kwenye mchezo dhidi ya Msumbiji huku kila mtu akiamini kuwa tumeshinda kwa mabao 2-1 na kuganga yajayo, wachezaji wetu wakafanya makosa dakika za mwisho na matokeo kuwa sare ya 2-2.

Unaweza ukaona ni makosa ya kibinadamu, lakini ukitoa majibu ya kisayansi ni kwamba robo tatu ya wachezaji waliocheza kwenye mechi ile hawana misingi mizuri ya soka; hawakuandaliwa kama wanasoka.

Mpaka mwanzoni mwa miaka ya 1990, Tanzania ilikuwa na wachezaji wachache sana au hakuna kabisa kutoka nje ya nchi, leo hii wako kibao na kuondoka na mamilioni ya fedha ambayo yangewekezwa kwenye soka la vijana sidhani kama tungekuwa tunafikiria kusajili mchezaji kutoka nje.

Matumizi makubwa ya fedha katika kusajili nyota wa kigeni yamekwenda mpaka kwa wachezaji wetu, mchezaji mmoja mwenye kiwango cha kawaida tu anasajiliwa kwa Sh milioni 70 huku vikosi vya pili vya timu hizo havina hata bajeti inayoeleweka hali inayothibitisha dhihaka katika kuendeleza mchezo wenyewe.

Uganda, Kenya, Rwanda na nchi zinazotuzunguka, klabu zake haziwezi kutoa mamilioni ya fedha kusajili mchezaji kutoka nje ya nchi na badala yake zenyewe zinawekeza katika soka la vijana na ndio maana kila msimu klabu zetu zinarudi huko kusajili.

Kifikra inabidi tubadilike hasa upande wa klabu kwani Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), halimiliki wachezaji, bali wachezaji ni mali ya klabu na hii ni kwa manufaa ya timu zetu za taifa.

RIPOTI ya 15 kuhusu uchumi wa Tanzania ya ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi