loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kocha atamba Yanga imeiva

Kwa mujibu wa tovuti rasmi ya Yanga, kocha huyo alisema licha ya kuwa na kikosi hicho kwa wiki moja, lakini ameona mabadiliko kiuchezaji na hivyo hana wasiwasi wa kufanya vizuri katika michuano inayomkabili ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha huyo aliyasema hayo baada ya mechi ya kirafiki dhidi ya Simurq PIK inayoshiriki Ligi Kuu ya Azerbajain ambapo timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2 mjini Antalya nchini Uturuki ambako Yanga iliweka kambi ya mazoezi kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.

“Timu imecheza vizuri nawapongeza vijana kwa kujituma, hakuna lisilowezekana katika mpira, wachezaji wangu sasa hivi wanajiamini na wanajua wanatakiwa wafanye nini kwa wakati muafaka, ilikua mechi nzuri sana hata kocha wa Simurq PIK amefurahia uwezo wetu,” alisema Mholanzi huyo.

Awali, Yanga ilikwenda huko na Kocha Msaidizi Charles Boniface Mkwasa kabla ya kuungana na Pluijm katika wiki ya mwisho, mara baada ya kutangazwa kurithi mikoba ya Ernie Brandts aliyefukuzwa.

Timu hiyo inatarajiwa kurudi nchini kesho kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Jumamosi wiki hii ambapo itaikabili Ashanti United.

Kwa mujibu wa tovuti ya Yanga, mechi dhidi ya Simurq PIK ilichezwa kwenye viwanja vya Hoteli ya Side Star mjini Antalya, hoteli hiyo ndiyo ulipofikia msafara wa Yanga.

Mchezo wa juzi dhidi ya Simurq PIK ulikuwa wa nne kwa Yanga tangu kuwasili Uturuki ambapo imeshinda michezo miwili dhidi ya Ankara Sekerspor 3-0, na Altay SK 2-0 zote za Ligi Daraja la Pili nchini Uturuki kabla ya kutoka sare na timu ya KS Flamurtari ya Ligi Kuu nchini Albania.

Mabao ya Yanga juzi yalifungwa na Didier Kavumbagu na Mrisho Ngassa.

KLABU ya Simba  imetambulisha  mashindano mapya ya Super  Cup, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi