loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kocha JKT Mbweni afungiwa mwaka mmoja

JKT Mbweni iliweka mpira kwapani zikiwa zimebaki dakika chache kabla ya mchezo kumalizika wakati ikicheza na Filbert Bayi Foundation (FBF) katika mchezo wa mwisho wa Ligi Daraja la Kwanza kwenye Uwanja wa Sokoine jijini humo.

FBF ilitetea ubingwa wake baada ya kuifunga JKT Mbweni ktika mchezo huo ambao mchezaji wa JKT Mbweni, Evodia Kazinja alitoka na mpira nje ya uwanja kabla ya muda kumalizika.

Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa Chaneta, Annie Kibira alisema kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokutana hivi karibuni, kilimtia hatiani Ramadhani kuwa alisababisha vurugu siku hiyo.

Hata hivyo, baadhi ya wadau wa netiboli wanahoji sababu za kumfungia Ramadhani badala ya timu ya JKT Mbweni ambayo hivi karibuni ilishiriki mashindano ya Muungano yaliyofanyika Zanzibar na kutwaa ubingwa huo, kwani ndio ilihusika na vurugu hizo.

Kwa mujibu wa Kanuni za Chaneta, timu inayosusa mchezo hufungiwa na inaweza hata kushushwa daraja, adhabu iliyotakiwa kutolewa kwa JKT Mbweni ambayo baadhi ya viongozi wake wamepewa onyo kwa vurugu hizo.

Hata hivyo, Kibira alisita kuwataja viongozi hao wa JKT Mbweni na waamuzi waliopewa barua za onyo kwa madai kuwa kufanya hivyo kutaiharibia timu hiyo.

Alisema maamuzi hayo yalifikiwa na kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokutana jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na hayo pia kilifanya tathmini ya mashindano hayo ya Ligi Daraja la Kwanza.

KOCHA Mkuu wa Coastal ...

foto
Mwandishi: Cosmas Mlekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi