loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Kocha JKT Ruvu akiri kibarua kazi ngumu

Kikosi hicho ambacho kina idadi kubwa ya vijana, kilicheza mechi ya kirafiki hivi karibuni na Ndanda FC na kufungwa mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam.

Akizungumza na 'Habarileo', Kondo alisema hadi kuanza kwa Ligi Kuu Septemba 20, mwaka huu watakuwa wamepata kikosi ambacho ni sahihi, kitakachowawezesha kufanya vizuri.

“Tuko katika maandalizi makubwa ya Ligi, tunaendelea kuangalia ni wachezaji gani ambao watatuwakilisha vizuri, tuna kazi kubwa ya kuchagua wale ambao wataonesha juhudi,” alisema Kondo.

JKT Ruvu tangu imeanza kujifua kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao, imeshacheza mechi za kirafiki na Azam FC na hivi karibuni Ndanda ambazo zote walipoteza, hivyo, wana kazi kubwa msimu ujao wa ligi kwani inategemewa kuwa ya kiushindani.

Katika msimu uliopita, timu hiyo ya Mkoa wa Pwani, ilimaliza katika nafasi ya saba ikiwa na pointi 31.

Kuelekea michuano ya Ligi Kuu, imesajili wachezaji wengi vijana wakiandaliwa kwa ajili ya kutimiza malengo yao kama sio kuchukua ubingwa wabaki salama ili kutoshuka daraja.

RUVU Shooting, Kagera Sugar na Gwambina ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi