loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kocha: Stars tayari kwa vita

Kocha: Stars tayari kwa vita

Taifa Stars ikiwa na wachezaji 26, wakiongozwa na Nooij na Kocha Msaidizi Salum Mayanga, waliwasili jana jijini Dar es Salaam wakitokea Mbeya ambako waliweka kambi tangu mwanzoni mwa mwezi huu.

Akizungumza baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Nooij alisema kikosi cha wachezaji wote kiko vizuri na kwamba wana matumaini ya kufanya vizuri.

“Maandalizi ni mazuri, wachezaji wameimarika na kikubwa ambacho tunategemea katika mchuano huo, ni kupambana kwa ajili ya kushinda ili tuweze kusonga mbele,” alisema kocha huyo Mholanzi.

Nooij alisema Zimbabwe sio timu rahisi, ni timu ngumu yenye wachezaji wazuri, lakini hawaiogopi kwa vile wamejiandaa vizuri kushinda.

Alisema anategemea kufanya mabadiliko katika kikosi chake wiki hii kwa kuweka wachezaji ambao watapambana na kuleta ushindani ili kujitengenezea mazingira mazuri katika mechi ya marudiano.

Alisema wataendelea na mazoezi kesho na keshokutwa kisha kuchagua wachezaji wazuri watakaoshuka dimbani Jumapili wiki hii. Baada ya mechi hiyo, watarudi tena jijini Mbeya kwa maandalizi ya marudiano.

Taifa Stars itacheza na Zimbabwe katika mechi hiyo ya kwanza ya Afcon na baadaye marudiano yatafanyika jijini Harare na mshindi atacheza na mshindi kati ya Msumbiji na Sudan Kusini, na mshindi kuingia katika hatua ya mwisho ya makundi kuelekea Morocco.

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi