loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kocha wa tenisi kuongeza wasichana

Akizungumza na gazeti hili, kocha huyo alisema timu yake ina wachezaji wengi vijana wa kiume katika umri kuanzia miaka 12 hadi 16 tofauti na wasichana ambapo wengi wameangukia katika umri chini ya miaka 12.

“Mwaka huu tumepata changamoto tulikosa wasichana katika umri wa miaka 14 na 16, inatubidi tutafute vijana wengi wa kuongezea katika timu yetu ya Taifa, tunaamini wapo wengi hawajapata watu wa kuwahamasisha,” alisema Kipingu.

Alisema atawatafuta wasichana kwa kutembelea kwenye shule mbalimbali na kutoa elimu ya mchezo huo, bila kubagua shule lengo likiwa ni kutafuta vipaji kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Kipingu aliongeza kuwa alifurahishwa na kikosi cha timu ya Tanzania kwa kufanya vizuri na kuiwezesha nchi kupanda katika nafasi ya pili katika ubora wa mchezo huo Afrika Mashariki.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Tenisi Tanzania (TTA), Fina Mango alisema mpango wa kutafuta wachezaji katika mikoa ufanyika kama kliniki hasa kwenye mikoa yenye viwanja.

Alisema wakati mwingine hushindwa kupata wachezaji kwa sababu hakuna viwanja vya kuchezea mchezo huo, hivyo ni changamoto kwao kutafuta njia mbadala za kuwasaidia kutimiza malengo yao.

“Mchakato wa kutafuta wachezaji tutaanza na Morogoro, tutatembelea mikoa michache kwanza, kisha tuendee mingine, naamini wakati ujao mambo yatakuwa mazuri, tutashika nafasi ya kwanza,” alisema.

TIMU ya Ruvu Shooting imeboresha kikosi ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi