loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kongamano la Uwekezaji Ukanda wa Ziwa Tanganyika Oktoba 26

Hayo yalisemwa mjini hapa jana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano la uwekezaji la Ukanda wa Ziwa Tanganyika, litakalofanyika mjini Sumbawanga kuanzia Oktoba 26 hadi Novemba Mosi mwaka huu.

Alisema baada ya makongamano ya uwekezaji kwenye Ukanda wa Ziwa Tanganyika yaliyofanyika miaka iliyopita wawekezaji kadhaa wameonesha nia ya kuwekeza katika ukanda huo wa mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma.

Alisema baadhi yao wametembelea mkoa na halmashauri kwa lengo la kupata taarifa zaidi na kuona maeneo husika.

Alisema orodha ya wawekezaji waliopo Mkoa wa Rukwa pekee na kila halmashauri zake ni 56 na kati ya hao walioanza kuwekeza ni 39 na wapatao 17 wanaendelea na taratibu za uwekezaji katika hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na hatua za umilikaji wa ardhi.

Alisema kutokana na mazingira ya Ukanda wa Ziwa Tanganyika kuna fursa kubwa za kufanya biashara za kimataifa kati ya Tanzania na nchi za Kongo, Burundi na Zambia.

Alisema mikoa ya Ukanda wa Ziwa Tanganyika ina fursa nyingi za uwekezaji ambazo bado hazijawekezwa ipasavyo ikiwemo sekta za viwanda, madini, kilimo, mifugo, uvuvi, maliasili, afya, elimu, utamaduni, michezo, usafiri na usafirishaji kwa njia ya barabara, anga na majini, katika Ziwa Tanganyika.

Pia vivutio vya kihistoria vinavyohitajika kuhifadhiwa na kuendelezwa, vivutio vya kitaliii ikiwemo Maporomoko ya Kalambo, samaki wa mapambo, mbuga za Lwafi, Katavi, Gombe na Mahale pamoja na mabwawa ya asili ya Kwela, Sundu na Chimchemi ya Majimoto.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi