loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Kortini kwa kuingiza vifaa nchini bila leseni

Attwi ambaye ni mfanyabiashara wa Kariakoo, alipandishwa kizimbani mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka yanayomkabili na Wakili Mwandamizi wa Serikali Tumaini Kweka, mbele ya Hakimu Mkazi Frank Moshi.

Kweka alidai kati ya Novemba 3, 2013 na mwezi Julai 2014 mshtakiwa huyo alifanya udanganyifu wa matumizi ya mtandao kinyume cha sheria.

Alidai kuwa mshtakiwa kwa nia ovu na udanganyifu aliingiza nchini vifaa vya mawasiliano ya kimataifa vyenye njia namba 2143281001701 bila ya kuwa na leseni zinazotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Wakili huyo wa Serikali alidai kuwa katika kipindi hicho, mshtakiwa bila ya kuwa na uhalali kisheria, aliingiza nchini na kuvifunga vifaa vya kielektroniki bila ya kuwa na kibali cha TCRA kinachomruhusu kufanya kufunga vifaa hivyo.

Aidha, alidai kuwa mshtakiwa huyo alitumia mitambo hiyo ya kielektroniki ambayo ilikuwa haijathibitishwa na TCRA.

Mshtakiwa pia anadaiwa kusababisha hasara ya Sh2,168,100,000 kwa TCRA kati ya Novemba 2013 na Julai 2014 kwa kutumia njia za huduma za mawasiliano ya kimataifa bila ya kuwa na leseni ya TCRA.

Hakimu Moshi aliiahirisha kesi hiyo hadi Agosti 11, 2014 kwa ajili kutajwa baada ya mshtakiwa kuyakana mashtaka hayo na upande wa mashtaka kudai kuwa upelelezi haujakamilika.

Mshtakiwa huyo, hakuruhusiwa kuzungumza chochote kwa sababu mahakama ya hakimu ya Kisutu haina mamlaka ya Kuisikiliza kesi hiyo bila ya kuwepo kwa kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP). Pia alipelekwa rumande kwa kuwa mahakama hiyo haiwezi pia kumpa dhamana hadi Mahakama Kuu.

foto
Mwandishi: Flora Mwakasala

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi