loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kuchapiwa siri ya ndani haina maana mbaya- Mavoko

Kuchapiwa siri ya ndani haina maana mbaya- Mavoko

Wimbo huo ulioimbwa na msanii Rich Mavoko ni wimbo unavuma kwa sasa huku ukiwa unapendwa zaidi kutokana na maneno yaliyogusiwa kwenye wimbo huo. Ni wimbo ambao unahusiana na masuala ya mapenzi huku ukiwa umekuja na mtazamo tofauti kuanzia ujumbe na hata mtiririko wa wimbo wenyewe.

Mavoko ni kijana ambaye amekuwa akifanya vema kwenye medani ya muziki ambapo anazo nyimbo nyingi kwa sasa. Ana nyimbo kadhaa, lakini kwa wafuatiliaji wa muziki, wimbo wa Marry Me ndio hasa uliomtambulisha kwenye soko la muziki kwani ndio uliovuma kuanzia mwishoni mwa mwaka juzi mpaka mwaka jana, baadhi ya nyimbo zake nyingine ni Silali na One Time.

Katika mahojiano hayo maalum, Mavoko anazungumzia wimbo wa Roho Yangu na kusema kuwa hakutarajia kama wimbo huo ungepokelewa kwa shangwe na mashabiki wa muziki. Anasema kuwa aliamua kuuimba wimbo huo kutokana na kugundua kuwa wapo watu wengi wanaotatizwa kwenye mapenzi na wanashindwa kujitoa katika mahusiano hayo.

Anasema kuwa wapo ambao wanakumbwa na visa vingi ikiwamo kudanganywa na mengineo lakini bado tu wanaendeleza masuala ya mahusiano. Anasema kuwa hiyo ndio moja ya sababu zilizofanya kuutunga wimbo huo wa Roho Yangu. Anasema kuwa ni wimbo ambao una maana kubwa ingawaje kuna watu ambao wamekuwa wakiuchukulia kwa maana tofauti au wakizingatia kipengele kimoja zaidi.

Katika wimbo huo kuna maneno ambayo ndio hayo ambayo Mavoko anasema kuwa yanachukuliwa tofauti. Maneno kama vile mjini msingi kiuno, kuchapiwa siri ya ndani na maneno kama vile Ujanja kunywa supu ya pweza. Anasema kuwa ni maneno ambayo yalikuwa kwa muda mrefu yakitumiwa lakini hayakuwahi kupewa kipaumbele kwa kuonekana kuwa ni maneno yenye maana gani zaidi.

Anasema kuwa msemo kama vile mjini msingi kiuno ni hakuwa na maana kuwa anawaelekeza watu kujiingiza kwenye ngono kibiashara kwa maana ya kutumia mwili wao kujiletea maendeleo. Ila anafafanua kuwa maana yake ni kuwaelezea baadhi ya vijana tena wakiume ambao wanatumia miili yao kama ndio msingi.

Akiwa na maana kuwa wanalelewa na kutunzwa na wanawake huku wao mtaji wao ukiwa ni viuno vyao. “Najua nikisema Roho Yangu ndani yake kunakuwa na ujumbe wa aina mbalimbali, kama vile kuwaasa mengi vijana na watu katika suala zima la mapenzi hapa nikiwa na maana kuwa yale ambayo nimeyagusia humu yanatakiwa kueleweka kiumakini zaidi,”anasema Mavoko.

Anaendelea kufafanua kuwa hata akisema kuwa ujanja ni kunywa supu ya pweza anawalenga kuwasaidia wale vijana ambao hawana uwezo mkubwa wa masuala ya mapenzi. Anasema kuwa kwa kuhakikisha kuwa wanalinda heshima zao ni kuhakikisha kuwa wanakunywa supu ya pweza na ndio maana amesema kuwa ujanja ni kunywa supu ya pweza.

Mavoko pia anautetea ujumbe usemao kuchapiwa ni siri ya ndani, ambao kwa sasa unaonekana kutajwa tajwa sehemu mbalimbali na watu wanaonekana kuuchukulia ni kama ujumbe muhimu katika maisha ya mahusiano. Mavoko anaongeza kuwa iwapo kama mtu akijikuta anakutana na masahibu kama hayo anachotakiwa kufanya ni kutambua kuwa hiyo ni kama suala jingine na kulitatua kwa ndani ya mazingira husika.

Anasema kuwa wapo watu ambao wanayachukulia masuala kama hayo ya kukuta mpenzi, mchumba au mke kutembea nje ya ndoa na wanaanza kuyangumza kwa marafiki au watu wengine badala ya kuifanya siri ya ndani. Anasema kuwa akisema kuwa kuchapiwa ni siri ya ndani hana maana kuwa wanatakiwa wakae kimya na kuyachukulia masuala hayo kama ya kawaida, bali iwe siri ya ndani na itatuliwe kwenye misingi ya kifamilia zaidi.

Akizungumzia maisha yake anasema kuwa kwa sasa ana mchumba wake ambaye sio mdau wa mziki kabisa. “Mimi natarajia kuoa na kwa sasa nina mtu wangu ambae ndio ninapanga nae maisha huyu ni mwanadada ambae kwanza haendekezi haya masuala ya muziki na sio mdau sana wa shughuli hizi,”anasema Mavoko.

Anaongeza kuwa yeye ni msanii ambaye analenga kuwa na familia bora atakayemheshimu mkewe na familia yake kwa ujumla. Gazeti hili lilipotaka kufahamu upande wa pili wa maisha yake binafsi kama msanii anapenda kitu gani na kipi hatumii kabisa Mavoko ‘alifunguka’… “Sipendi kunywa pombe wala kuvuta sigara mimi ni msanii ninayetumia muda wangu mwingi kukaa ndani kujifunza zaidi muziki”.

Anaongeza kuwa hiyo inamsaidia zaidi kujiweka karibu na watu mbalimbali na kupata mawazo ya nyimbo mpya za kuimba. Anaongeza kuwa kwa sasa amejenga nyumba kubwa kwa wazazi wake mkoani Morogoro na pia amenunua gari ambalo analitumia kwa maisha yake.

“Muziki umenisaidia kununua gari, kupata shoo nyingi nje ya nchi hasa kwa mwaka huu wa 2014 tayari nimeshaweka kwenye ratiba hiyo ya kwenda nje ya nchi kama Uingereza na kwengineko,”anasema Mavoko. Anatumia fedha zake nyingi katika kuvaa na kuhakikisha kuwa anakuwa na mwonekano wa kisanii kila mara.

Anaongeza kuwa yeye anajitambua kama msanii makini na mwenye nia ya kufika mbali na ndio maana hata wimbo wake wa Roho Yangu ameutengenezea video yenye umakini wa hali ya juu. Anasema kuwa alilazimika hata kurekodi kwa kutumia Kamera ya kisasa zaidi kutoka Kenya huku akiwa na mwongozaji wa utengenezaji wa video ya wimbo wake huo kutoka Uganda.

Anaamini kuwa umakini ndio kitu ambacho kinaweza kumsaidia msanii kufika mbali kikazi zaidi. Aidha Mavoko kwa upande mwingine alimkumbuka msanii marehemu Khamis Mkiety, ‘Sharomilionea’. Anasema kuwa msanii huyo alikuwa rafiki yake mkubwa na mtu wake wa karibu zaidi na kuongeza kuwa kifo chake kinaendelea kumuuma hadi sasa.

OFISI ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) ni Taasisi ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi