loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

'Kuna tatizo kwenye mfumo wa elimu'

Wakizungumza na wanahabari hivi karibuni, viongozi wa baraza hilo lenye makao yake makuu mjini Iringa wamesema ipo haja kwa wadau wa sekta hiyo kukubaliana ni lugha ipi kati ya Kiingereza au Kiswahili itumike kufundishia tangu ngazi ya elimu ya awali.

“Kuna shida katika mfumo wetu, mtoto anafundishwa kwa lugha ya Kiswahili chekecheka hadi darasa la saba na baada ya hapo lugha inabadilika masomo mengi anasoma kwa Kiingereza,” alisema Mwenyekiti wa TACELAM, Chelestino Mofuga.

Mofuga alisema hali hiyo imewafanya wanafunzi wengi wajikute katika mazingira ya kushindwa kumudu lugha ya Kiingereza hata wanapohitimu mafunzo ya vyuo vikuu.

“Ni muhimu tukaangalia suala hili kwa kina, kama ni Kiswahili basi kitumike toka shule ya msingi hadi chuo kikuu na kama ni Kiingereza iwe hivyo hivyo,” alisema.

Katibu wa TACELAM, Dk Newton Kyando alisema; “mfumo wa matumizi ya lugha zote mbili unawaweka wasomi wengi njia panda ya kushindwa kuyafafanua mambo kwa lugha tofauti na ile waliyomalizia.”

Akitoa mfano, Dk Kyando alisema; “Profesa wa kemia anaacha matumizi ya Kiswahili katika somo hilo baada ya kuingia kidato cha kwanza jambo linalompa shida ya kufafanua mambo mbalimbali kuhusu somo hilo kwa lugha ya Kiswahili.”

Novemba 4-6, baraza hilo linatarajia kuendesha kongamano la kimataifa linalolenga kuwajengea uwezo watoto katika ushiriki wa masuala ya sayansi na teknolojia.

RAIS John Magufuli amewataka wasaidizi wake ...

foto
Mwandishi: Frank Leonard, Iringa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi