loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kundi la Five Star lavunjwa

Akizungumza na 'Habarileo' juzi mmiliki wa kundi hilo lililodumu kwa miezi tisa tangu liibuke upya Sharif Mambo ‘Shakti’ alisema kuwa, ameamua kulivunjilia mbali kundi hilo baada ya kuchoshwa na wasanii wake.

Shakti alisema kuwa pamoja na kulianzisha kundi hilo kutokana na mapenzi yake katika muziki wa taarab, lakini amekuwa akikerwa na tabia za baadhi ya wasanii wake kudai vitu ambavyo havipo hata katika mkataba.

Alisema kuwa alikuwa akijitahidi hata kuwalipia kodi ya nyumba na chakula wakati hilo halipo katika mkataba na asipomlipia, msanii hafiki mazoezini anakwambia atafanyaje kazi hajala au hana pa kulala.

Alisema kuwa alikuwa na mkataba wa miaka miwili na wasanii wa kundi hilo, lakini ameridhika kuwaachia ili aondokane na matatizo ya wasanii ambayo awali alikuwa akiyasikia kwa wengine tu na hakufikiri kama wanaumiza kichwa namna hiyo.

Tayari baadhi ya wasanii wameondoka na kutua katika makundi mbalimbali kama Dar Modern ambapo Mwamvita Shaibu na Mwanahawa Ally wametua katika kundi hilo.

Kundi hilo liliibuka upya mwaka jana baada ya mwaka juzi wasanii wake 13 kufa katika ajali mbaya ya gari, wasanii hao ni Issa Ally Kijoti, Sheba Juma, Tizzo Mgunda, Omary Hashim, Omary Abdallah, Haji Mzania, Nassoro Madenge, Husna Mapande, Hamisa Omary, Maimuna Makuka, Hassan Ngeleza, Ramadhani Maheza na Ramadhani Mohamed.

Hata hivyo, kiongozi wa wasanii wa kundi hilo Ally Jay alisema bado hajapewa taarifa kuhusu kuvunjwa kwa kundi hilo, lakini alikataa maelezo kuwa limevunjwa sababu ya usumbufu wa wasanii na kusema kuwa, huenda mmiliki ameyumba kiuchumi.

“Bado sijapata taarifa rasmi lakini najua lazima mmiliki ataniita maana mimi ndio muanzilishi lakini si kweli kuwa wasanii ni wasumbufu nafikiri huenda ameyumba kifedha,” alisema Jay ambaye ni miongoni mwa wasanii wachache walionusurika kwenye ajali iliyoua wenzao 13.

KLABU ya Simba  imetambulisha  mashindano mapya ya Super  Cup, ...

foto
Mwandishi: Cosmas Mlekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi