loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kundi la Weusi lilivyopania kufanya makubwa 2014

Kundi la Weusi lilivyopania kufanya makubwa 2014

Tayari makundi mawili ya wanamuziki wanaofanya muziki huo yameungana ili kufanya kazi zao pamoja kukwepa wizi huo. Makundi hayo kutoka mkoani Arusha, moja likitambulika kama Nako 2 Nako lenye makazi yako Kaloleni ambapo mwanzo lilikuwa likiundwa na Ibra De Hustler , Isic Maputo ‘Lord Eyes’ na George Sextus ‘G Nako’.

Wakaungana na kundi la Liver Camp, ambalo lenye makazi yake Daraja Mbili likiundwa na ndugu wawili Dickson Simon ‘Niki wa Pili’, na John Simon ‘Joh Makini’. Kuungana kwa makundi hayo mawili, ndipo likazuka Kundi jipya la Weusi ambalo kwa sasa ndilo kundi ambalo linafanya vizuri kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya katika mtindo wa Hip Hop.

Akizungumza katika mahojiano maalum na gazeti hili, mmoja wa wanamuziki wa kundi hilo ‘G Nako’, anasema kwa sasa kundi hilo lina wasanii watano, akiwa Lord Eyes, Nikki wa Pili, Joh Makini na Bonta. Anasema kuungana kwa makundi hayo na kutokea kwa kundi hilo, ni kukusanya nguvu ili kuweza kukabiliana na tatizo ambalo limekuwa likiwakuta wanamuziki wa Hip Hop.

Akizungumzia kuhusu matamasha, anasema kwa sasa tayari wameshaanzisha kampuni ambayo imesajiliwa kwa jina la Weusi, huku wakiandaa matamasha yao wenyewe.

“Sasa hivi tumekuwa tukiandaa matamasha yetu, na kila kitu tunafanya wenyewe,” anasema. Anasema katika kuandaa matamasha huwa wanakutana na changamoto nyingi, kutokana na kampuni nyingi zimekuwa zinasuasua juu ya kuwaunga mkono. Hivyo kutokana na kampuni hizo kutokuwa na ushirikiano wa moja kwa moja, wamejikuta wakiandaa kwa fedha kutoka mfukoni mwao.

G Nako anasema changamoto nyingine katika kuandaa tamasha, huwa wanakumbwa na wasiwasi, kama fedha zao zitarudi au laa hasa kutokana na kila kitu kutoka kwenye mikono yao. “Ujue kuandaa kitu kwa fedha zako kunahitaji moyo, kwakuwa unakuwa unawekeza fedha nyingi tatizo lipo katika kurejea kwa fedha hizo,” anasema.

Kuhusiana na tatizo la wasanii wengi wa Hip Hop kulalamika nyimbo kutopewa kipaumbele kama muziki mwingine, G Nako anasema umeshapita muda wa kulalamika, ilimradi kila msanii ajue njia gani azitumie ili kazi yake ifike kirahisi kwenye vyombo vya habari. “Muda wa kulalamika umeisha, kila mtu anajua ni jinsi gani ya kufikisha kazi zake kwenye vyombo vya habari na kupigwa kwa kazi zao,” anasema.

Anasema wao kazi zao zimekuwa zikichezwa kwenye redio na runinga mbalimbali bila ya wasi wasi kwakuwa wamekuwa wanafanya kazi nzuri. Pia msanii huyo anasema katika kampuni hiyo, ya Weusi kwa sasa wanatengeneza fulana ambazo wanasambaza kupitia maduka makubwa ya nguo, na zingine wanasambaza kwenye vyuo ambapo wana mashabiki wengi.

“Huwa tunawauzia jumla watu wenye maduka makubwa na wao wanauza kwa bei wanazotaka wao, popote pale,” anasema. Zaidi ya T-shit anasema kwa sasa kampuni hiyo, imeshaanza kujipanga kutengeneza, kofia, soksi, nguo za ndani na nguo zingine kwa ajili ya kuzisambaza zaidi kila sehemu.

Anasema lengo lao kwa sasa kampuni hiyo kuweza kuitanua na kufanya vitu vingi, na sio kutegemea muziki kwa kila kitu, kwakuwa mziki wenyewe unaenda na kubadilika.

Kuhusiana na watu ambao wamekuwa wakidhamini kutengeneza kazi zao, kama muziki na video ambazo kwa sasa ‘zimekuwa na gharama kubwa, G nako anasema kupitia kampuni yao, wamekuwa wakisaidiana kuandika nyimbo, na huwa wanapeana nafasi ya kutoa wimbo jambo ambalo linawafanya waendelee kubaki kileleni kwa muda mrefu.

Hivyo anasema hata video zao, pia huwa wanashirikiana kufanya moja baada ya nyingine na kukamilisha kwa muda muafaka. “Huwa tunasaidiana na washikaji katika kukamilisha video zetu, lakini kwa kiasi kikubwa sana wahusika tunakuwa wenyewe,” anasema. Anasema kwa sasa kampuni yao inaandaa video nne, mbili wanafanyia Arusha na mtayarishaji Nisha, ambapo kwa sasa wapo kwenye hatua za mwisho.

Anasema baada ya hapo wanatarajia kufanya video ya wimbo Bei ya Mkaa, ambapo watafanya na Adam Juma wa Next Level. “Video mbili zingine ikiwemo Nikumbatie, ingawa bado hatujajua tutafanya na nani, ila nategemea mtayarishaji atatoka nje” alisisitiza G Nako. G nako anasema kupitia Kampuni yao ya Weusi, wamekuwa wakijiepusha na mabifu, au ugomvi ambao kwao hauna tija.

Anasema, ugomvi ndio umekuwa ukirudisha nyuma muziki wao, na hata wale wanaousikiliza wanaona kama wote wahuni na ndiyo maana hata mara ya kwanza walikuwa na vikwano vyingi kwa wazazi. Anasema kwa sasa kampuni yao itaendelea kusimamia matamasha yao, na kuangalia vyanzo vingine vya mapato ikiwemo miito ya simu.

Akizungumzia mgogoro wa biashara ya miito ya simu, anasema, hilo linatokana na wasanii kufanya kazi kubwa lakini wanunuzi wanachukua fedha nyingi. “Biashara ya Ringtone (miito ya simu) inatoka sana watu wananunua, lakini tukija kwenye kugawanya fedha zilizopatikana wao wanachukua mapato mengi, na ukiwauliza watakuambia kuna vijikato vidogo vidogo kama kodi na vingine,” anasema.

OFISI ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) ni Taasisi ...

foto
Mwandishi: Mohamed Musa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi