loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kwa hili, Edward Lowassa tutakukumbuka daima

Alisema: “Ninapokuwa safarini katika mikoa mbalimbali huwa nakutana na wanafunzi wanaokwenda au kutoka shuleni. Huwa najiuliza, kama siyo shule za sekondari za kata, wangekuwa wapi wanafunzi hawa?”

Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli anasema aliwahi kukutana na binti mmoja aliyeshindwa kujizuia na hata kuamua kumwambia wazi wazi kuwa, kama siyo shule hizi alizoziasisi Lowassa, msichana huyo sasa angekuwa baamedi lakini sasa, zimekuwa mkombozi wake.

Lowassa hana budi kukumbukwa na Watanzania katika kipindi cha uhai wake, hata atakapomaliza safari yake duniani kwani alilowafanyia Watanzania, ni la wema na asiyekubali ni yule mwenye hulka ya “kutembea kichwa chini miguu juu” pekee kwa kugeuza hata mazuri kuwa mabaya.

Ninasema hivyo huku nikikumbuka namna nilivyokuwa mmoja wa waliozikejeli shule hizi za kata kwa kuziona zisizo na faida hata nilipo w a h i kumuuliza Rais J a k a y a Kikwete pale Ikulu Dar es Salaam naye akajibu akisema, kujenga shule ni hatua nzuri ya awali.

Kwa majibu ya Rais Kikwete nikakubali kuwa, isingekuwa rahisi kuwa na shule zenye walimu, vitabu, maabara na miundombinu bora, bila kwanza kuwapo shule hizo hivyo, kazi ya ujenzi wa shule imefanyika, sasa kinachofuata ni kuboresha shule hizo.

Ninayasema hayo ninapokumbuka miaka ya nyuma namna suala la watoto “kukanyaga” sekondari lilivyokuwa muujiza na kitendawili kilichokuwa wazi kwa watoto wachache kupindukia huku hao nao bila kujali uwezo wao, jamii ikaamini kuwa ni watoto wa vigogo pekee waliofaulishwa kwa “mbinu”.

Si kwamba katika kipindi cha nyuma watoto hawakuwa na akili darasani, bali hapakuwa na nafasi za kutosha kuwachagua hivyo, walishinda mitihani lakini hawachaguliwi kutokana na ufinyu wa nafasi.

Sekondari za kata zimekuwa mkombozi wa wanyonge zikiwezesha watoto waliokosa nafasi, kupata nafasi za kusoma sekondari na siyo siri, wengi wameendelea vizuri hadi kufikia ngazi za vyuo vikuu na hao, ni wale ambao kama zisingekuwa sekondari hizi ambazo wengine wanakosea kiasi kwamba, wanazibeza na kuziita majina ya kejeli, ama wangevuta bangi, dawa za kulevya na hata kujitumbukia katika uhalifu mbalimbali.

Katika harambee hiyo ambayo zaidi ya Shilingi milioni 233 zilipatikana zikiwa ni pesa taslimu na ahadi, Lowassa mwenyewe alisema, “Ukereketwa wangu katika suala la elimu na hasa shule hizi za kata, ni dhihirisho sahihi la umakini wa sera za Chama Tawala (CCM)” Lowassa amefanya na anaendelea kuwafanyia wema Watanzania kiasi kwamba ingawa haombi shukrani, Watanzania wenyewe wanapaswa kuuona wajibu wa kumshukuru na kumuombea zaidi kwa Mungu.

Kama alivyosema siku hiyo, shule nyingi za vijijini na hata zilizo pembezoni mwa miji mikubwa kama Dar es Salaam, suala la elimu liko nyuma na hali hiyo, imeifanya hata mikoa na maeneo hayo kuwa nyuma kielimu na kimaendeleo. Hata hivyo, kimantiki, uwepo wa shule za sekondari katika kila kata ya Tanzania, umesaidia kuleta usawa wa kielimu katika mikoa yote nchini.

Katika harambee hiyo ya kuchangia upatikaji wa vifaa na elimu bora katika shule 12 za sekondari za kata katika Tarafa ya Mbagala, Dar es Salaam, Lowassa mwenyewe alichangia shilingi milioni 10 huku Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile naye akichangia kiwango hicho.

Harambee hiyo ilienda sambamba na uzinduzi wa mahafali ya shule hizo ambazo ni pamoja na Chamazi, Mikwamba, Nzasa, Changanyikeni, Mbande, Kingugi, Malela, Saku, Toangoma, Mbagala na Mbagala Kuu.

Mpango huu alioufanya Lowassa huko Mbagala akishirikiana na Dk Ndugulile (Mbunge wa Kigamboni), ni ishara wazi kuwa viongozi hao wametambua kuwa kazi ya ujenzi wa shule imefika pazuri, sasa umebaki wajibu wao kwa kushirikiana na wadau na wananchi wote, kuziwekea shule hizo mazingira mazuri ya kutoa na kupokea elimu.

Ndiyo maana Dk Ndugulile alisema katika uchangiaji huo kuwa, “Nawaombeni kwa dhati kuwa tushirikiane kulifanya zoezi hili liwe endelevu katika juhudi za ku nyanyua elimu yetu maana si tu kwamba hili ni jukumu la serikali, bali jukumu letu sote tukiwamo waziwazi kwani kutoa ni moyo na wala si utajiri hivyo, tuendelee kujitoa kwa dhati kwa ajili ya manufaa yetu na kizazi chetu kijacho.”

Alichokisema Lowassa kuwa CCM, Serikali, wazazi na wadau wote wanaowapenda watoto na kizazi chao, wanao wajibu wa kuwatafutia vijana (watoto) maendeleo yao ni kweli hivyo, hawana budi pia kubadilisha mazingira ya shule zao na kuyafanya bora zaidi kutolea elimu bora kupitia uchangiaji wa hali na mali.

Ndiyo maana Lowassa alisema, “Tunahitaji watoto wetu wapate elimu bora inayojibu mahitaji ya sasa kwa masomo yanayotoa nafasi katika ajira maana ajira ya vijana ni jambo la msingi.” Akaongeza, “Vurugu katika nchi nyingi duniani, ni matokeo ya vijana kupata elimu mbovu hivyo ni vema sote tuisadie Serikali kutoa elimu bora na hata walimu, nao tuwasaidie kwa kuwasikiliza kero na madai yao ili tusigombane nao na badala yake, tuwasikilize ili watimize vema wajibu wao.”

Mwandishi wa makala haya ni mchangiaji wa gazeit hili (0752 008080)

“MTU niliyefanya naye mahojiano alikuwa anafanya kazi kwenye ...

foto
Mwandishi: Joseph Marwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi