loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Kwa wanawake: Huddah, Prezzo sasa paka na chui

Awali yalikuwa ni ‘mapambano’ kati ya msichana huyo Mkenya na binti Mtanzania, Loveness Malinzi a.k.a Diva wakati mtangazaji huyo wa kipindi cha Ala za Roho katika kituo cha redio cha Clouds FM alipokuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki huyo.

Upepo sasa umebadilika, sasa ni ‘vita’ ya maneno kati ya Prezzo na Huddah a.k.a The Bossy Lady, walikuwa na uhusiano wa kimapenzi, wameachana, na sasa wanatukanana kwenye mitandao ya kijamii.

Inadaiwa kuwa, chanzo cha ugomvi wa Prezzo na msichana huyo ni uhusiano wa sasa wa kimapenzi kati ya Prezzo na msichana mwingine Mtanzania, Starlisha Tillya a.k.a Chagga Barbie, a.k.a Stess free lady. Inadaiwa kuwa mwanamke huyo ni mfanyabiashara, anaishi Marekani, na anamiliki pia gazeti tando (blog) www.tanzaniteglamour. blogspot.com.

Inadaiwa kuwa jina halisi la mwanamke huyo ni Stella, na kwamba, hadi mwezi Agosti mwaka huu alikuwa na uhusiano na mwanamuziki Bracket wa Nigeria. Kwanza yalikuwa ‘mapambano’ ya Huddah na Mtanzania huyo anayeishi, Minnesota Marekani, lakini sasa ‘vita’ imehamia kwa Prezzo, ambaye sasa anasema, alikuwa na msichana huyo kwa ajili ya ngono tu.

Kwa mujibu wa Prezzo, hakukuwa na jambo la zaidi kati yake na mshiriki huyo wa BBA 2013 zaidi ya kupeana naye mikono, kupiga picha kwa ajili ya vyombo vya habari, na ngono. Mwanamuziki huyo amesema wakati anahojiwa na Heads Up, kuwa, amefanya ngono na Huddah takribani mara tatu, na kwamba, msichana huyo amekasirika kwa sababu yeye (Prezzo) hakutaka kuendelea na uhusiano naye.

“Tulikuwa pamoja kama mara tatu na nadhani alipenda alichokipata. I’m addictive kwa hiyo hakupenda niondoke” amesema Prezzo na kudai kuwa, Huddah alikuwa anawabughudhi wanawake wote waliokuwa na uhusiano naye (Prezzo) akiwemo Diva, Goldie (sasa ni marehemu) na sasa Chagga lakini yeye (Prezzo) hakusema chochote.

“Huddah ni kama mali ya Serikali, amelala na karibu dunia nzima, unadhani Rais angeweza kutulia na mwanamke kama huyo,” anauliza Prezzo na kufafanua kwamba, Huddah alikuwa mshirika wake kwa ajili ya ngono tu. Mwanamuziki huyo ameyasema hayo kujibu mapigo ya Huddah ambaye ameandika kwenye mtandao wa Instagram kuwa, Prezzo a.k.a King of Bling ni mtoto wa mama na amefilisika.

Kashfa za Prezzo zimemkera Huddah, naye kajibu mapigo kwa kusema, ni bora kuwa mali ya serikali kuliko kuwa mtoto wa mama. Kwa mujibu wa msichana huyo, anamshangaa mwanamuziki huyo yupo bize kumtukana, alidhani angeendelea na maisha yake, aache kutukana wanawake ambao hawana hisia naye, na kwamba, hamhitaji.

Kwenye ukurasa wake kwenye mtandao wa Instragram Prezzo anasema, inafurahisha kwa namna mambo ya nyuma yasivyomsumbua, na amemkaribisha Huddah kwa kusema ‘…welcome to my future’ Huddah amemjibu kwa kusema, “Una future gani wewe? mwanaume mzima hela hauna, @ Prezzo 254, umefilisika na bado unaishi kwa mama yako... wacha kujiaibisha, sitaki nikuaibishe mbwa koko. Respect yourself (jiheshimu)!’ Huddah anatukanana na Prezzo zikiwa zimepita siku chache tangu msichana huyo apambane kwa maneno na mpenzi wa sasa wa mwanamuziki huyo, Starlisha. Msichana huyo Mtanzania amekiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Prezzo. Wakati wa malumbano ya Huddah na Mtanzania huyo, Mkenya huyo alihamasisha ‘jeshi’ la kumsaidia kwenye mapambano hayo, wakajitokeza wasichana kadhaa kutoka Tanzania na Kenya wakaifanya kazi hiyo kwenye mitandao, na wakapongezwa kwa kazi nzuri waliyoifanya. “Asanteni nyote kwa kumpasha yule shuga mami habari ya mjini. Ahahahaha! Nimecheka sana, yaani anikome kunitaja na kunitusi kwenye instagram yake!!! Amesema Huddah kwenye mtandao wa Instagram. Mapambano ya mshiriki huyo wa BBA na Chagga ni muendelezo wa hali kama hiyo na wanawake waliokuwa na uhusiano na Prezzo akiwemo Diva ambaye aliamini angefunga ndoa na mwanamuziki huyo, lakini sasa hataki kuuzungumzia uhusiano huo. Diva kaomba watu wasiandike chochote kuhusu Huddah au Prezzo kwenye ukurasa wake kwa kuwa ukurasa huyo umefungwa muda mrefu na hataki malumbano. “Huwa nafuta na kujisikia vibaya nikiona mnaendelea kuandika kuhusu Prezzo. Ukweli ni kuwa moyo wangu upo kwa mwanaume mwingine na Tattoo ya jina lake katika mkono wangu itafutwa, nalifanyia kazi” “Ninamheshimu, ni mtu mzuri, lakini tafadhali jina lake kwenye ukurasa wangu inatosha, natumaini mmenielewa, nawapenda wote,” anasema Diva. Kabla ya penzi la Diva na Prezzo kuingia shubiri, mtangazaji huyo mara nyingi alikuwa anaandika kwenye mitandao kumsifu mwanamuziki huyo na kuwalaumu waliokuwa wakizungumzia uhusiano wao wakiwemo waliomtuhumu Prezzo kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengi. “Watu wananizungumzia sana mimi na Prezzo na wengine wanasema eti ni mtu wa wanawake sana, jamani Prezzo ni Rais, ni mtu mzima na labda hamumjui vizuri ila niamini mimi, jamaa ni sweetheart,” alisema Diva. “Ni mtu mzuri sana na naweza kusema nina bahati sana kuwa naye. Acheni kuzusha vitu ambavyo havipo na hata kama vipo hamna uhakika navyo. Hilo la kusema anatembea na Huddah au Victoria, namtakia kila la heri, ana baraka zangu zote na nampenda kwa kuwa ni mwanaume wa aina yake, niacheni,” alisema mtangazaji huyo wa Clouds FM ya Dar es Salaam. “Prezzo ni mwanaume, tena mwanaume wa Kiafrika, maneno ya nini?...namna ninavyojisikia ni mpango wa Mungu, kila mtu anafahamu mimi ni mwanamke wake, ni mtu pekee ninayemhitaji, habari ndio hiyo. sibadiliki and haachwi mtu,”alisema Diva. “Mimi namshangaa huyu dada anayeniandama kwenye mtandao toka aliposikia nipo na Prezzo, kwa kifupi kwa Prezzo nimefika na ndoa muda si mrefu utapita ili tuweze kuishi kama mke na mume,” alisema Diva. Tovuti ya http://www.ghafla. co.ke ilimemkariri Diva akisema, Prezzo ni Almasi yake angani, anamfanya awe na furaha, ni kipenzi chake na atachora tatuu ya jina la mwanamuziki huyo ili awe anatabasamu siku nzima kila siku na kwamba, hicho ndiyo kitu alichokihitaji kwa wakati huo. “Mapenzi ni upofu, kijana wa Nairobi kanichanganya na tatuu itanifanya nijisikie vizuri. Kwa uzuri au ubaya, jina lake litakuwa moyoni mwangu” amekaririwa Diva na kwamba, kama penzi lake na Prezzo halitadumu, itakuwa heri pia, lakini ule ulikuwa muda wake, alihisi yupo kwenye mapenzi mazito na kamwe hatajuta. Siku chache baada ya Diva kuyasema hayo, Mahakama Kuu nchini Kenya ilivunja ndoa ya Prezzo ikiwa ni miezi kadhaa baada ya kutengana na mkewe, Daisy Jematia Kiplagat, na kukawa na taarifa zilizodai kuwa alipanga kumuoa Diva. Mke wa Prezzo, aliomba talaka mahakamani kutokana na kile alichodai kuwa ni mateso, manyanyaso na kwamba, msanii huyo anayejiita Mfalme wa Bling, CMB Prezzo, pia alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengine na alikuwa akimpiga. Mahakama Kuu jijini Nairobi imekubali kuivunja ndoa ya Prezzo, na imetoa amri kuwa, rapa huyo awe anatoa shilingi 50,000 za Kenya kila mwezi kumtunza mwanawe aliyezaliwa Machi 2009. Prezzo na Daisy walifunga ndoa Desemba mwaka 2008 Karen Country Lodge. Katika ushahidi wake, Daisy aliieleza Mahakama Kuu kwamba, Prezzo aliisaliti ndoa yao kwa kuzini na wanawake kadhaa na akamtaja mmojawao kuwa ni mwanamitindo wa zamani, Joy Wanjohi. Alidai kuwa, Prezzo alikuwa anamnyanyasa kwa maneno na kumsababishia msongo wa mawazo. Ilidaiwa mahakamani kwamba, Prezzo pia alikuwa anampiga Daisy na hakutimiza wajibu wa kutoa fedha za kuihudumia familia yake. Mama huyo alidai pia mahakamani kuwa, mwanamuziki huyo alikuwa analewa sana pombe, sanjari na kutumia dawa za kulevya takribani kila siku na baada ya kulewa alikuwa anamtukana na kumpiga. Mwandishi wa gazeti la Standard alimhoji Prezzo Januari mwaka 2012, akasimulia kuhusu matatizo kwenye ndoa yake, na uhusiano wake na mwanamitindo wa zamani, Wanjohi. Prezzo aliiwakilisha Kenya katika shindano la Big Brother Africa mwaka 2012, na wakati akiwa katika jumba hilo, inadaiwa kuwa alianzisha uhusiano na mwakilishi wa Nigeria, Goldie Harvey. Goldie alifariki dunia Februari 14 mwaka huu jijini Lagos nchini Nigeria baada ya kuugua kwa muda mfupi. Imeandikwa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali.

BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA) ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi