loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Leo siku ya kuombea taifa

Aidha, suala la mchakato wa Katiba mpya litaombewa pia na imeelezwa kuwa, bila amani, uzalendo na amani ya kweli, maridhiano hayataweza kupatikana kwa kuwa kila upande utakuwa unajali maslahi binafsi na si ya Taifa.

Katika maombi hayo yatakayofanyika kwenye Kituo cha Sala na Maombezi cha Emaus kilichopo Ubungo kinachoratibiwa na Chama cha Kitume cha Karismatiki Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.

Katibu wa Karismatiki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Merdad Banzi aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, maombi hayo kwa Taifa ni maalumu kuuombea mchakato wa Katiba mpya, amani na utulivu, Uchaguzi Mkuu ujao na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Banzi alisema kabla ya maombi hayo yatakayofanyika leo mchana katika viwanja vya kituo hicho cha sala kilichopo nyuma ya stendi ya mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani, pia watatembelea vituo vya watoto yatima, magereza ya Ukonga, Keko na Segerea pamoja na vituo vya wazee wasiojiweza.

Alisema pia watatembelea hospitali za Mwananyamala, Temeke, Amana, Muhimbili na Ocean Road ambako kote huko watatoa misaada mbalimbali kulingana na mahitaji wa walengwa pamoja na kuomba nao kuwatia moyo kwamba Mungu hajawaacha na anawapenda.

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Kondoa kwa tiketi ya Chama ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi