loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

LHRC yataka Waziri Kagasheki ajiuzulu

Kinadai Waziri Kagasheki kupitia operesheni hiyo ya Tokomeza Ujangili, aliamuru watuhumiwa wa ujangili, wateswe na kuuawa pindi watakapopatikana, jambo ambalo ni kinyume na haki za binadamu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Maboresho na Utetezi wa LHRC, Harold Sungusia alisema waziri huyo hivi karibuni alitoa tamko la kuvitaka vyombo vinavyohusika na kulinda maliasili, kuwapiga risasi na kuwaua wote watakaokutwa wakijihusisha na ujangili.

Alisema tamko hilo, lilifuatiwa na operesheni hiyo ya safisha majangili, ambayo tangu kuanza kwake nchi nzima, imekuwa ikikiuka haki za binadamu, kutokana na watu wanaokamatwa na kutuhumiwa na kosa hilo, nyumba zao zimekuwa zikichomwa moto, mifugo yao kuuawa na wengine kupoteza masiha.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa kituo hicho, Hellen Kijo-Bisimba, Sungusia alisema LHRC imepokea baadhi ya taarifa kutoka sehemu mbalimbali, zikiwemo za kifo cha Emilia Muro aliyekuwa mke wa mtuhumiwa ujangili, Elias Cosmas na mifugo 190 kupigwa risasi katika maeneo mbalimbali yaliyo jirani na hifadhi za taifa.

Alisema kituo hicho paoja na kumtaka Kagasheki ajiuzulu, pia kimetaka wahusika wote wa operesheni hiyo ya tokomeza ujangili yaani askari wa maliasili wachukuliwe hatua kali za kisheria na Serikali iwalipe fidia wale wote walioathirika na operesheni hiyo.

Hivi karibuni katika mkutano wa 13 wa Bunge, unaoendelea mjini Dodoma, baadhi ya wabunge waliijia juu Serikali na kumtaka Kagasheki ajiuzulu, kutokana na operesheni hiyo ambayo walidai imesababisha maafa makubwa kwa wananchi hasa wa jamii ya wafugaji.

Kutokana na hoja hiyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, aliagiza Serikali kutoa taarifa kwenye Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuhusu operesheni hiyo.

Tayari Makinda ameunda Kamati Teule ya Bunge kwa ajili ya kushughulikia mgogoro wa muda mrefu wa wakulima na wafugaji nchini.

RAIS John Magufuli amesema Manispaa ya Ilala imepandishwa ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi